ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 15, 2013

NAPINGA WABUNGE KWENDA JKT

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu (wa pili), akikagua gwaride la askari wapya 822 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakati wa kufunga mafunzo yao ya miezi sita kwenye uwanja wa Mlale JKT jana. Kushoto ni Kamanda wa gwaride hilo Meja Aman Ramadhan.

Na Liberatus Mwangombe/ Raia
Tahadhari!!!!!Tumia akili zaidi kuliko HISIA kuelewa kilicho andikwa hapa, unaweza kuwa na mawazo tofauti na yangu, ni sawa. This is how democracy works.

NAPINGA WABUNGE KWENDA JKT
Nimesikia kwa muda kuwa wabunge watajiunga na JKT. Nilipata kuona baadhi ya comments kuwa ni wazo zuri, LAKINI, nitaomba kutofautiana na wengi kwa sababu zifuatazo;

Mosi: Ni KUJIONGEZEA GHARAMA kitaifa kuwaweka hawa watu JKT. Sina uhakika ni kiasi gani watakua reimbursed (sijui kama watalipwa posho!!!) wakiwa mafunzoni. Lakini obvious kutakuwa na gharama za vyakula, malazi n.k. Je, Ikitokea vita watakuwa FRON LINE, kwa maana nyingine, tunaweza kuwatumia vitani au kwa ulinzi? THEY GONNA SPEND FOR NOTHING- HATUWEZI KUWATUMIA FRON LINE.

Pili: Jeshi na siasa ni vitu viwili tofauti. Hatutaki itokee chama chochote kiingize ITIKADI zake jeshini. Hili la kuliangalia kwa makini. Kumbuka, wanamapinduzi wengi wametumia jeshi kueneza itikadi zao na kufanya mapinduzi.

Tatu: Mbunge ni muwakilishi wa wananchi na inabidi atumie muda mwingi kuwasiliana na wanainchi ili ajue kero zao na kuhimiza maendeleo jimboni mwake. Kwenda JKT atleast inabidi atumikie miezi sita. Fanya hesabu.

Nne: Kama ni uzalendo wa kweli, ilipaswa wajiunge na jeshi wakiwa vijana au kabla hawaja anza kuwatumikia wananchi. Na maanisha kama JKT ilikuwa haipo, wangejiunga hata na Polisi au Jeshi la ulinzi la Tanzania (JWTZ). Kuna viongozi ambao walipitia JKT, lakini hawana uzalendo na ni MAFISADI number one. Tazama nchi zilizo endelea, wanapita Jeshini kwanza na baadaye wanaanza kuwatumikia raia kwa kuwarepresent bungeni n.k. Mfano, John Mcain, senator in USA, au John Kerry ambaye sasa ni Secretary of State America.

Tano: Nimeona wanatoa sababu ya kujiunga na jeshi kuwa ni kujifunza kazi za kila siku za maisha, kiuchumi, kijamii na nidhamu. Guys! Give me a break. Kama umeshakua Mbunge na unategemea kwenda kujifunza nidhamu ukiwa bungeni, tafadhari kaa chini na re-think. Uchumi na mambo ya kijamii, kwa nini usisome vitabu na research kwa wananchiunao waongoza.

Sita: Kama wanataka kujiweka fit, kwa nini wasibadirishe style ya maisha. Kula vizuri, kuacha sigara, kupunguza pombe, kujiunga na gym, na kuelekeza nguvu zaidi kwenye kuwatumikia wananchi.

Mwisho: Naomba mh. Raisi aingilie swala hili na kusitisha ili kuokoa GHARAMA, MUDA na NGUVU za waTanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka Liberatus, nimekupata straight na nakuunga mkono. Wabunge wa TZ wameshakithiri na ukosefu wa upeo wa kufikiri, inasikitisha....Mdau Haji Jingo, California.