Sunday, February 17, 2013

PADRI WA KANISA KATOLIKI APIGWA RISASI ZANZIBAR

Padri Evarist Mushi
Padre wa Kanisa la Katoliki la parokia ya Minara Miwili lililopo mji mkongwe, Zanzibar, Padri Evarist Mushi  amepigwa risasi ya utosini na kufariki papo hapo na watu wasiojulikana.

Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi hii (kwa saa zaTz) kwenye kanisa la Mt. Theresia na akiwa eneo la Mtoni ndipo alisimamishwa na watu wawili waliokuwa wamepakizana katika katika pikipiki aina ya  vespa wakampiga risasi.

Mashuhuda wanasema, baada ya tukio hilo gari hilo liliacha njia na kugonga nyumba moja iliyokuwa karibu na kanisa hilo.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali kuu ya Zanzibar iliyopo Mnazi Mmoja.  Sababu za kupigwa risasi kwa Pari huyo bado hazijafamika.

Matokeo haya ya kihalifu yanayozidi kuendelea kutokea Zanzibar ni jambo la kusikitisha sana.
Tutaendelea  kuwajuza kwa kila taarifa itayopatikana.

3 comments:

Anonymous said...

ISLAM = CHUKI
.....ukipenda amani au ustaarabu kwa namna yoyote hauwezi kuwa Muislam safi; ... kwa sababu hautoweza kutekeleza yanayofundishwa ktk Quran.

...Wonder why serikali inakaa kimya ????

Anonymous said...

Hawa watu wa Mungu wanahitaji police escort now. This is the second time nimesikia mtumishi wa Mungu kapigwa risasi. Serikali iamke!!!

Anonymous said...

To anonymous Feb. 17. Ni kwa kigezo gani unaweza kuthibitisha kwamba waliomuua ni waislamu?. Mushi ni mtu ambae kaishi Zanzibar kwa miaka mingi sana bila ya kuhukumiwa kwa imani yake. Ukiristo iliingia Zanzibar mwanzo kuliko hata kwenu bara. Religious tolerance ni ustaarabu uliojengeka tokea Enzi. Zanzibar tunapinga sana kuvamiwa na mijitu iliyokosa ustaarabu ambao Leo hii wanachufua jina na sifa za Zanzibar. Wazanzibari hatuna tabia za kuchukiana na kuuana kwa risasi . Wacha shutuma za dhidi ya imani za watu wa dini Fulani.