Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova |
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa polisi imeanzisha mapambano dhidi ya vikundi vinavyotumia vibaya itikadi za kidini na kisiasa ili kuvuruga amani.
Aliwataka viongozi na wafuasi wao kuondokana na tabia ya kufanya vitendo vinavyoleta hofu kwa wafanyabiashara, wawekezaji, watumishi wa umma, taasisi na wananchi kwa jumla.
Alisema matendo yote ya kuwatia hofu wananchi yanaharibu utaratibu wa kawaida wa maisha pamoja na kuleta madhara ya kiuchumi, kisiasa, uhuru wa kuabudu pamoja na kuwabadilisha watu kimawazo na kisaikolojia.
Alisema kutokana na kujitokeza kwa matishio dhidi ya viongozi wa dini zote kushambuliwa pamoja na kuuawa, Jeshi la Polisi limeweka mtandao maalumu katika namna, ambayo linashirikiana kwa karibu na viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha maisha na mali pamoja na taasisi zao zinakuwa katika hali ya usalama.
“Katika hili tunaahidi kupambana na mtu yeyote atakayetishia uhuru wa kuabudu pamoja na kuwaletea hofu wahusika. Kinachotakiwa ni kuzidisha ushirikiano kati ya viongozi wa dini, waumini wao pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi. Tutaanzisha ngazi ya mtaa hadi makao makuu ya jeshi la polisi,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Mimi hawa watu waanishangaza siku zote. Wao ikitokea habari za machafuko ndiyo wanajipanga wakati siku zote wako tu wanajihusisha na ujambazi pamoja na rushwa.
Post a Comment