Wednesday, February 6, 2013

PUNDA AFANYA UNYAMA AMNG'ATA MTOTO

Picha ni Mtoto Fransi Mgogi akipewa huduma ya kwanza na Muuguzi wa zamu Hirido Mligo katika kituo cha Afya Migoli.
Punda aliyefanya unyama huo huyo hapa
MTOTO ang'atwa na punda mkono wake wakati akicheza jirani na punda huyo katika eneo la Migoli Mtera wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12;30 jioni katika kijijini Migoli baada ya Punda huyo kumng;ata mtoto mdogo wa kiume mwenye miaka 6 wa kijiji hicho .
Punda huyo akiwa mitaani akizurula bila utaratibu ilivyo kawaidayao katika maeneohaya alikutana na Mtoto Fransi nakumkamata mkono wake wa kushoto kwa kinywa chake na kumning’iniza juu akikimbia nae mpaka wananchi walipo msogelea kwa mayowe na kipigo akamuachia.
Baba wa mototo Ndg Francis Mgogi akizungumza na muandishi kwamasikitiko makubwa alisema tukio hili nilaajabu lakini anawasiwasi na hal iya huyo Punda ingawa kunakawaida ya Punda kuzagaa bila kujulikana mwenyewe na huwezi muuliza mtu.

Akiwa katika kituo cha Afya Kope kataya migoli alipopelekwa mtoto huyo alipokelewa na Muuguzi wa zamu Hirida Mligo ambae alipokuwa akimpahuduma kwa bahati mbaya Umeme ulikuwa umekatika toka saa tisa jioni hiyo kukapelekea kuwa na giza katika chumba cha Upasuaji.
Ilimbidi muuguzi huyo kutumia taa ya mionzi ya jua ambayo ilikuwa na mwanga mdogo sana akiomba msaada wa kumulikiwa anapomsafisha eneolililo jeruhiwa akagunduo shimo kubwa lililo tokana na jino la Punda likionyesha Mfupa wa nyuma ya mkono juu ya Kiwiko.
Hali iliomfanya muuguzi kumshauli Mzazi akisha mpatia sindano ya kinga inabidi amkimbize mjini jambo lililo Mshitua mzazi huyo alisikika akisema uwezo wa kukodi Gari hana itambidi alale apande Basi asubuhi kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Kwa bahati mbaya muda wote huo Dr wa zamu alikuwa hajafika ingawa muuguzi wa zamu alimtuma mlinzi akamuite.
Akizungumza na muandishi Dada mmoja Esta John mkazi wa kijiji Migoli alisema Punda huyo kaisha fanya matukio zaidi ya hilo alishamuuma mbwa na kuuwa kabisa siku za nyuma na janayake amemuuwa Bata kwa kumkata shingo.
Juhudi za muandishi kumpata Dr wa mifugo kuthibitisha Uzima wa Punda huyo hazikufanikiwa alipofika nyumbani kwake na kupewa namba ya Simu ambayo alipompigia haikupokelewa. 
 (picha na habari na Saidi Ng'amilo )

No comments: