Mwanamuziki anayekubalika sana Afrika Mashariki kwa kazi zake ambazo wakati
wote zinakuwa zimebeba ujumbe mzito wa mafundisho, Samba Mapangala amerekodi
wimbo maalum unaojulikana kama Chagua, kwa ajili ya kuwahamasisha wakenya
kushiriki katika uchaguzi wao kwa amani pamoja na kuchagua viongozi makini.
Ujumbe wa msanii huyu ambao umepakiwa katika kibao kikali cha miondoko ya
"Sokous" kwa mujibu wake mwenyewe, ni mchango wake katika kuhamasisha amani
nchini Kenya, nchi ambayo ndipo mahali alipokulia.
Kazi hii imerekodiwa huko Arlington, Virginia pamoja na Paris, na tayari
imeshaanza kusambazwa kwa njia ya mtandao, na ujumbe wake pia ni wa manufaa kwa
nchi nyingine za Afrika ambazo mara nyingi hupitia hali zinazofanana hasa
nyakati za uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment