ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 20, 2013

SENTENSI 5 KUHUSU NIGERIA KUVUNJA REKODI KWA RAIA WAKE WANAOISHI NJE YA NCHI


Stori kutoka London ni kwamba imefahamika wanigeria wanaoishi nje ya nchi hiyo wametuma nyumbani kiasi cha dola za kimarekani bilioni 21 mwaka uliopita, kutokana na hilo Wanigeria hao wameingia kwenye tano bora ya nchi tano ambazo raia wake wanaongoza kwa kutuma pesa nyumbani.

Nchi ya kwanza ni India, Philippines inafata, ya tatu ni Mexico na ya nne ni Nigeria
Taarifa imeonyesha kwamba India na China kwa pamoja zimepokea dola za kimarekani bilioni 60 kutoka kwa raia mbalimbali wa nchi hizo wanaoishi nje ya nchi, Philippines ($24 billion), Mexico ($24 billion), and Nigeria ($21 billion).

Nchi nyingine ambazo zipo kwenye kumi bora ya raia waishio nje ya nchi kutuma pesa nyumbani ni pamoja na Egypt iliyoshika nafasi ya 6 ambayo mwaka jana raia wake walituma nyumbani $18.

Inaaminika ongezeko hilo limetokana na maisha kuwa magumu ndani ya nchi na raia kutegemea sana misaada kutoka kwa ndugu zao wanaoishi nje ya nchi pamoja na wanaorudi nyumbani kwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali hasa ya ujenzi.

No comments: