Friday, February 1, 2013

UBALOZI WA MAREKANI UTURUKI WALIPULIWA


Ubalozi wa Marekani kama unavyoona kwenye picha juu na chini umelipuliwa mapema Ijumaa Feb 1, 2013 mji mkuu wa Uturuki, Ankara na kuua watu wawili ambaye mlinzi wa Ubalozi huo raia wa Uturuki, na mlipuaji aliyekua amelivaa bomu hilo naye alikufa papo hapo na kujeruhi watu kadhaa waliokuwepo kwenye kitengo cha VISA. Kishindo hicho cha bomu kilifumua mlango wa kuingilia kwenye kitengo hicho na kuacha wingu la moshi likisambaa kwenye mtaa uliopo Ubalozi huo.
Akiongea mapema na waandishi wa habari, Gavana wa Mji wa Ankara, Alaaddin Yuksel alisema mlipuaji alikua tayari ameishaingia ndani kwenye chumba cha Kitengo cha VISA na mlipuko kuharibu vibaya kitengo hicho na kujeruhi watu kadhaa waliokuwemo ndani kwa maswala ya VISA
Balozi wa Marekani nchini Uturuki. Francis Ricciardone aliongea na waandishi wa habari waliofika Ubalozini hapo kudodosa mawili matatu ilikuweza kujua kulikoni. Francis Ricciardone alisema, anasikiktika kwa kumpotenza mlinzi wake na anashukuru Serikali ya Uturuki kwa kulichukulia swala hili kwa uzito unao staili mpaka sasa hizi haijulukani ni nani yupo nyuma ya mlipuko huu lakini wengi wanahisi Siria (Syria) inahusika na mlipuko huu.
Polisi wa Uturuki wakiwa kwenye tukio
Mmoja wa majeruhiri akikimbizwa Hospitali

No comments: