Polisi wa Kikosi cha Reli wamemnasa Feruzi Ally (73), akiwa na tani 23 za shehena ya mataruma ya reli aliyokuwa anaisafirisha kutoka Tabora kuileta Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Reli Saada Haji, aliiambia NIPASHE Jumapili kuwa, Ally alikamatwa na vipande 492 vya mataruma haya aliyokuwa ameyapakia kwenye kontena la urefu wa futi 40 mali ya kampuni ya kusaga nafaka ya Azania ya jijini.
Kamanda Haji alisema kati ya vyuma hivyo vipande 23 vilikuwa chakavu na vilivyobakia ni vizima na kuongeza kuwa alikamatwa akiwa maeneo ya Temeke baada ya upekuzi kufanywa kwenye gari lililokuwa na shehena hiyo lenye namba 772 AXN mali inayomikiwa na Azania na kwamba alikuwa ameyafunika na magunia 20 ya pumba za mahindi.
Alisema yalikuwa yanapelekwa kuuzwa kwenye viwanda vya kueyusha vyuma hasa vinavyotengeneza nondo.
Aliliambia gazeti kuwa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo alitoroka baada ya kukamatwa na kueleza kuwa alitumwa mkoani kupeleka bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo na wakati wa kurudi alikubaliana na mmiliki wa vyuma hivyo wavipakie ili gari lisirudi Dar es Salaam likiwa tupu.
Aliongeza kuwa uchunguzi unafanyika kujua mataruma hayo yamechukuliwa kutoka Tabora ama yameng’olewa kutoka stesheni ipi au yalichukuliwa kutoka sehemu gani.
Alisema kampuni hodhi ya reli (Rhoco) na polisi wanakokotoa thamani halisi ya mataruma hayo, licha ya kwamba Ally alidai yana thamani ya Sh. milioni 10 na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment