ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 25, 2013

Yaliyo Moyoni Mwangu Kuhusu Wasanii wa Bongo Flava Kusingiziana Uchawi

YAMOYONI:Shindano la mkali wa rhimes kama lingefanyika mwaka 2012 au 2013 nadhani tungesema Afande sele amechinja kondoo 100 wa kafara ili ashinde ama ameua albino,kipindi kile Juma nature anatamba na album yake ya ugali ,Ferooz na nyimbo yake ya ukimwi,Professor,Dully & Mr Nice kipindi kile wanaonekana miungu watu nadhani ingekua kile kizazi ni kizazi kama tulichonacho sisi kwasasa ungesikia hawa ni mafremason,mwingine angesema hawa ni wachawi wanatembelea nyota za akina.

Ngurumo, Jumbe, Shaban Dede ama mzee Issa Matona. Lakini kuonesha tofauti iliyokuwepo kati ya kizazi kile na hiki wale walikua wamekaa kimya kila mtu akijaribu kutafuta njia ya kupata mashabiki kupitia staili mbalimbali za kimziki. Amini ninachokwambia kuna tofauti kubwa sana kati ya kizazi kile cha mziki ule na kizazi hiki cha sasa cha kina Bob Jnr na Ney wamitego na ndomana kikaitwa kizazi kipya na upya umedhihirika. Sasa nirudi kwenye mada yangu.
Kwamimi ninachofahamu ni kwamba mganga ndo siku zote atakayekwambia nani anakuroga, na unapomsikia mtu anasema karogwa ujue alienda kwa mganga sasa jiulize alifuata nini? Hapa tunapause kwanza...... Hili suala la mtu anakurupuka na anamtaja msanii mwenzake anamroga yeye amejuaje? kama hajaenda kwa mganga?

Hapa unagundua ule ubunifu wa AY kufanya commercial, Dully na mwanasesere ama TMK kufanya Rap katuni wasanii wasasa wamekosa na ndomana wanatafuta mbinu mbadala ya wao kujulikana. Nategemea nione wasanii wakitumia mda huu kuandika nyimbo kali ili watanzania wawaelewe na pia wafanye video nzuri ili wavuke boda lakini bado baadhi yao hawafanyi mazuri yakuwasaidia bali wanajenga malumbano na maneno yasiojenga mziki wetu.USHAURI wangu kwa wasanii ni wawe na uvumilivu, waheshimiane na wafanye kazi ili sisi mashabiki tufurahi na tuelimike pia.

Tukumbuke pia mziki ni ajira kwa watu wengi sio wenye vipaji vya kuimba na producers tuu, tujue kua kuna kuzaliwa na kuna kufa, binadamu sote sawa tumeumbwa kwa mfano wa yeye tunaemuamini haya ya duniani yakupita tu tuyaache yapite sisi tupendane maisha yaendelee. Yangu yalikua hayo tuu kwa leo nawatakia kazi njema ndugu WANDEWA STREET 4 LIFE c.e.o ally stly

No comments: