Dereva Jackson Simbo (43), anayedaiwa kuingilia msafara wa Rais Jakaya Kikwete na kusabisha kifo cha askari wa Kikosi cha Usalama barabarani jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kusomewa mashtaka matatu.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislous Komanya, alimsomea mshtakiwa huyo mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kwey Lusemwa.
Komanya alidai kuwa Machi 18, mwaka huu barabara ya Bagamoyo katika mataa ya kuongozea magari eneo la Bamaga jijini, Dar es Salaam, mshtakiwa aliingilia msafara wa Rais Kikwete.
Ilidaiwa kuwa Simbo ambaye pia ni Mfanyabiashara mkazi wa Mbeya akiwa kwenye gari lenye namba za usajili T.328 BML aina ya Land Lover Discovery alisababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa aliingiliza msafara kinyume cha kifungu namba 43 kidogo cha (1)63 kidogo cha (2) na (1) kifungu cha 27 kidogo cha (1) (a) cha usalama barabarani.
Ilidaiwa katika shtaka la tatu kuwa baada ya matukio hayo, mshtakiwa hakutoa taarifa polisi alitoweka kusikojulikana.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka.
Mahakama ilimtaka awe na wadhamini wawili wa kuaminiwa watakaosaini hati ya Sh. milioni mbili na alitimiza masharti hayo.
Komanya alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kesi itasikilizwa maelezo ya awali Aprili 15, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:
Huyu dereva katika picha ni kweli umri wake ni miaka 43?
Post a Comment