ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 18, 2013

AZAM FC WAMVAA SHAFII DAUDA KWA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI DHIDI YAO

UONGOZI WA SSB na Azam FC umesikitishwa na makala iliyotolewa na Blogu ya Shaffihdauda eti, klabu zimekuwa zikidhulumiwa na SSB na Azam FC kwa mechi zao kurushwa Live na Star TV.
Tungependa ieleweke kuwa Azam FC ingependa kuona mashabiki wake nchini na nje ya nchi wakiiona mechi live na ndiyo maana tumekuwa tukilipia matangazo hayo, pia tunadhani hili ni jambo jema la kuungwa mkono na wadau.
Pia tungependa ifahamike kuwa kwenye kipengele cha mkataba kati ya SSB na Star TV, kuna kipengele kinachoilazimisha Star TV kutoa sehemu ya pato lake na kuvilipa vilabu ambapo kwa mechi moja klabu hupata shilingimilioni moja (1,000,000)
Kwa mechi zinazochezwa chamazi, klabu hupata mgao wa kiingilio wa chini ya shilingi laki tatu hivyo nyongeza ya milioni moja kwa mechi kurushwa live ni pesa ya kutosha angalau kwa kuanzia
biashara ya haki ya matangazo ya TV lazima ianzie mahali flani na Azam FC inajaribu kuonesha njia kwa klabu ndogo ndogo ambapo hii ni fursa kwa Star TV na Klabu husika kujaribu kuboresha hali hii badala ya kupiga majungu. Tunashukuru kuwa kumekuwa na uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa klabu.
Ubaya wa habari yenyewe ni pale walipoinukuu klabu ya JKT Ruvu kuwa ililalamika kwa shaffihdauda.com, huu ni uongo na uzandiki mkubwa kwani JKT Ruvu walishapokea malipo yao kupitia kwa katibu wake Bw. David Ngaga ambaye alipokea pesa na kusaini vocha ya malipo ya Sh. 1000,000/-. Angalau wangeitaja Polisi Moro kwa kuwa malipo yao yalikuwa yakiandaliwa na kwa makubalano nao yatafanyika siku ya Jumanne 19/03/2013
Tungependa kutoa rai kwa waandishi wa habari kufanya uchunguzi wa taarifa zao kabla ya kukurupuka na kuibuka na makala zenye hisia za migogoro, uchochezi na majungu

No comments: