Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa |
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Kinondoni, zimesema kwa sasa hazina mpango wa kutoa fedha zozote kuwasaidia watu waliokumbwa na mafuriko wanaoendelea kuishi mabondeni.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akizungumza katika mahojiano na Radio One katika kipindi cha Kumepambazuka jana, alisema serikali imekuwa ikisisitiza watu wanaoishi mabondeni wahame, lakini wapo ambao wameendelea kukaidi agizo hilo.

“Tumewatangazia mara kadhaa watu wanaoishi mabondeni wahame kutokana na hali hiyo kwa sasa hatutakuwa na maamuzi yoyote ya kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo kusaidia watu waliokumbwa na mafuriko,” alisema Silaa.
Naye Meya wa Manisapaa ya Kindoni,Yusuf Mwenda, alisema mafuriko yanayotokea katika Wilaya ya Kinondoni, yanatokana na baadhi ya watu kutupa ovyo takataka ndani ya mifereji ya kupitishia maji na katika mto Msimbazi.Alisema kutokana na uchafuzi huo, halmashauri imeunda timu ya watu kadhaa kuangalia namna ya kupanua mto Msimbazi.
Alisema katika kukabiliana na tatizo la mafuriko, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imepitisha azimio la kukataza watu kujenga mabondeni na atakayekaidi nyumba yake itabomolewa haraka.
Mameya hao walitoa wito kwa watu wanaoendelea kuishi mabondeni kuhama kutokana na uwezekano wa mvua za Aprili kuleta athari zaidi za mafuriko.
Mvua zilizonyesha tangu Jumamosi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam , zimesababisha adha kubwa kwa wakazi wake kutokana na nyumba zao kujaa maji na kulazimika kwenda kuomba hifadhi kwa ndugu na jamaa zao.
Waliokumbwa na kadhia hiyo, ni wale wanaoishi mabondeni ambao serikali mara kwa mara imekuwa ikiwapigia kelele kwa kuwataka kuhama katika maeneo hayo.
Baadhi ya maeneo ambayo mvua hizo zilileta athari na kusababisha mafuriko ni Tabata Relini na Kigogo huku eneo Zahanati ya Mwenge hadi Nakiete duka la dawa, maji yakijaa barabarani na kusababisha watu kupita kwa shida.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, akizungumzia mafuriko hayo kwa njia ya simu, alisema serikali alishatoa tamko la kuwataka wakazi wa mabondeni kuhama na kwenda sehemu nyingine na msimamo huo uko pale pale.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment