Waziri Harrison Mwakyembe |
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, ambayo imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 548; kwa ajili ya kushughulikia miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida, huku kipaumbele kikiwekwa katika ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege na usarifi wa reli, kwa mwaka mpya wa fedha wa 2013/2014.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 390. 5 zimetengwa kwa ajili ya kushughulikia miradi ya maendeleo, wakati Sh. bilioni 158.4,zimetengwa kwa matumizi ya kawaida.
Alisema kamati imepitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya kuridhishwa nayo, kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kidogo kwenye matumizi mengine.
Serukamba, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi na watendaji wa wizara hiyo, katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.Alisema katika fedha za maendeleo, Sh. bilioni 255.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege na usarifi wa reli.
“Bajeti hii ni nzuri kwa kuwa fedha nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Tofauti na miaka iliyopita fedha zilielekezwa kwenye matumizi ya kawaida. Matumaini yetu ni uboreshaji wa miradi husika,” alisema Serukamba.
Alisema pia Sh. bilion 12 zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wastaafu wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) waliokuwa wanaidai serikali kwa muda mrefu.
Vilevile, alisema katika bajeti hiyo, zaidi ya Sh bilioni 86 zitaelekezwa kwenye upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kituo cha tatu (teminal three).
Alisema katika mwaka wa fedha uliopita, kamati yake ilitoa mapendekezo mbalimbali, ambayo yameanza kufanyiwa kazi, ikiwamo upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati katika ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika.
Kwa mujibu wa Serukamba, mengine ni matengenezo ya meli katika ziwa Nyasa, Victoria na Tanganyika na uboreshaji wa usafiri wa treni za jijini Dar es Salaam, kwa kununua za kisasa kwani zilizopo zimepitwa na wakati.
“Usafiri wa Treni ni moja ya mapendekezo yetu. Na serikali imelifanyia kazi. Lakini tumeitaka kuboresha zaidi kwa kununua treni ya kisasa na si zilizopitwa na wakati,” alisema Serukamba.
Alisema yote yamefanyiwa kazi na kinachopaswa ni usimamizi thabiti kuhakikisha fedha zilizoelekezwa kwenye maeneo hayo zinatumika inavyotakiwa.
Hata hivyo, aliitaka serikali kupeleka asilimia 55 ya fedha za bajeti kwa mwaka uliopita ya wizara hiyo ili kuiwezesha kutekeleza majukumu iliyojiwekea kwa mwaka huo.
Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu mwaka wa fedha wa 2012/13 kumalizika, asilimia 25 ya fedha za ndani na asilimia 30 ya fedha za nje ndizo zimepelekwa wizarani humo.
“Tunaitaka serikali kulipa fedha za mwaka jana ili miradi ya maendeleo ya mwaka jana isikwame, imepita miezi tisa, Wizara haijapata fedha zote kutoka Wizara ya Fedha, imebaki miezi mitatu kumaliza mwaka wa bajeti, haya ni mapungufu” alisema
Kamati hiyo leo itaendelea na mapitio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2012/13 na 2013/14.

No comments:
Post a Comment