Maofisa upelelezi wadaiwa kutupiana mpira
Kova: Tunasubiri upelelezi kwenda kwa
Sakata la kukamatwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, limeanza ‘kuviumiza kichwa’ vyombo vya dola.
Lwakatare alitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinamzokabili, ikiwemo kutoa kauli zilizosambazwa kwenye mitandano ya kijamii, zinazohatarisha uvunjifu wa amani nchini. Hata hivyo, hakufikishwa mahakamani hadi muda wa mahakama kufanya kazi ulipomalizika, hivyo kumfanya aendelee kubaki ‘lupango’ hadi wiki ijayo.
NIPASHE Jumamosi ilifika kwenye viwanja wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu majira ya saa 6:35 mchana na kukuta baadhi ya wabunge wa Chadema wakiongozwa na timu ya mawakili wa mtuhumiwa Lwakatare wakisubiri mteja wao afikishwe mahakamani hapo.
Mawakili hao ni Wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatara na Mabere Marandu ambaye naye ataungana na jopo hilo mteja wao atakapofikishwa mahakamani.
Hata hivyo, hadi saa 2:46 Lwakatare alikuwa hajafikishwa kwenye viwanja vya mahakama hiyo kitendo kilichoilazimisha timu hiyo ya mawakili kutoa msimamo wao. Akizungumza kwa niaba ya mawakili wenzake, Lissu alisema kuwa, wamefika mahakamani hapo toka asubuhi wakisubiri mteja wao.
“Tulikuwa tunasubiri mteja wetu aletwe hapa ili ashtakiwe lakini kama mnavyoona waandishi hadi tunazungumza na nyie jambo hilo halijatekelezwa, baada ya muda kupita tumewasiliana na wahusika wa kesi hii na haya ndiyo majibu yao,” alisema.
Lissu alisema akiwa hapo aliwasiliana na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kigondo, ambaye masuala ya upelelezi wa Lwakatare yapo chini yake lakini alijibiwa yupo mkoani. “Nilimwambia nimeambiwa kuwa yupo Dar es Salaam na toka juzi yeye ndiye aliyekuwa akishinda na Lwakatare, akanijibu kuwa anayekaimu nafasi hiyo ya DCI ni Issaya Mungulu, “ alisema.
Lissu alisema baada ya Kigondo kumpatia namba ya Mungulu alimpigia simu naye akasema yupo mkoani Mtwara na kwamba masuala ya Lwakatare anayehusika ni Kigondo. Mungulu alimtaka Lissu ampigie baada ya nusu saa ili amweleze nini kinaendelea na baada ya wakili huyo kufanya hivyo, alielezwa kuwa Lwakatare anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo. Lissu alisema baada ya kukata simu ya Mungulu alimpigia Kigondo ambaye naye alimweleza kuwa, ameambiwa na wakubwa wake, mara baada ya kumaliza kazi yake, aipeleke huko.
Akieleza zaidi, Lissu alisema sheria za nchi zinasema ndani ya saa 24 mtuhumiwa anatakiwa kupelekwa mahakamani lakini wameshangazwa na kitendo cha jeshi hilo kuvunja sheria hiyo na kukaa na mteja wao siku tatu mfululizo. “Kitendo hichi kinaashiria kuwa, hawajui Lwakatare anashtakiwa na kosa gani na hawana uhakika wa kile wanaotaka kumshtaki nacho, tulitaka wamlete mahakamani ili awe chini ya usimamizi wa mahakama lakini hawajafanya hivyo,” alisema.
Aliongeza kuwa, jeshi hilo limekuwa chanzo kikubwa cha ukiukwaji wa sheria huku likijiona lenyewe lipo juu ya sheria hizo. “Lwakatare amekamatwa kwa mambo ya kushikizashikiza tu kwa sababu jeshi la polisi linaendeshwa kisiasa..
wanahofu na jopo la mawakili leo wangepita wapi,” alisema. Lissu alisema endapo Jumatatu mteja wao hatapelekwa mahakamani, wataenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ili awaeleze kama jeshi lake lipo juu ya sheria za nchi. Aidha, alisema wanachofahamu mteja wao hajafanya kosa lolote na kwa wale wanaoona anakosa wampeleke mahakamani.
Akijibu kauli ya Mbunge wa Iramba, Mwigulu Mchemba kuwa ana ushahidi wa viongozi wa Chadema wanapanga mauaji na kwamba ushahidi huo upo kwenye mitandano, Lissu alisema ameona video hiyo lakini haionyeshi hilo na kueleza kuwa wajiandae sawasawa. Naye Profesa Safari alimtaka IGP Mwema awaambie wanaomshikilia Lwakatare wampe dhamana.
Alitoa mfano wa mwanariadha Oscar Pistorius wa Afrika Kusini ambaye anakabiliwa na shtaka la kumuua rafiki yake wa kike, lakini alipewa dhamana na kuhoji kwa nini Lwakatare anyimwe haki hiyo. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipotakiwa kueleza sababu ya Lwakatare kutofikishwa mahakamani alisema hana taarifa kama alikuwa anapelekwa mahakani leo (jana).
Hata hivyo, alimtaka mwandishi asubiri ili awasiliane na makao makuu ya polisi kuthibitisha hilo ambapo baada ya muda alimpigia na kumweleza kuwa, anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni. Akaongeza kuwa, mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika, jalada litapelekwa kwa wakili wa serikali. “Yeye ndiye mwenye mamlaka ya kusema Lwakatare anakosa la kujibu au la, “ alisema.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment