
Kwa wiki tatu mfululizo nimekuwa nikielezea matatizo ya kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ‘kuruka ukuta’. Kutokana na mada kuwagusa watu wengi na kutaka kujua kama kuna tiba, nimeona nitumie wiki hii kuelezea tiba ya tatizo hilo.
Kwa kweli mada yangu ya madhara anayoyapata mwanamke anayeingiliwa kinyume cha maumbile imewashtua wanawake wengi ambao wameonekana kuchanganywa na mchezo huo ambao una madhara kwa asilimia 100.
Nimepata maswali mengi juu ya tiba ya mwanamke aliyeucheza mchezo huo, huku wengine wakionyesha wazi kuchanganyikiwa na hawajui hatima ya maisha yao baada ya kuufanya mchezo huo.
Kumekuwa na maswali mengi japokuwa mengi yalikuwa yakifanana. Wapo wanaofanya kwa shinikizo na wengine kwa starehe ambao hawakujua madhara yake.
Nitaandika maswali machache bila kutaja namba ili uone jinsi gani mchezo huo ulivyosambaa sana katika mapenzi ya sasa.
Msomaji 1: Mimi ni mama na mchezo huo niliufanya kama mara nne hivi, lakini siku nyingi kama miaka mitano iliyopita. Sijaufanya tena na wala siutaki, je, madhara uliyoelezea kwenye gazeti kama vile kulegea misuli wakati wa uzee nitayapata? Je, nitagunduaje nimepatwa na ugonjwa huo? Mungu wangu jamani nimekoma, sirudii tena.
Msomaji 2: Hii mada ya mwanamke kurukwa ukuta ina tiba na kama mchezo huo nimeuanza naweza kupona?
Msomaji 3: Habari, nimesoma makala yako katika Gazeti la Championi, je, kama nilifanya mapenzi kinyume cha maumbile nikaja kuacha kabisa nitasumbuliwa katika uzazi?
Maswali yalikuwa mengi na yalionyesha jinsi gani wengi hawakujua madhara yake na walitaka kujua tiba yake hasa ni nini.
Tiba yake ipo kwa mtu aliyeufanya mchezo huo kwa muda mrefu na kuacha. Tiba ya kwanza ni kuacha kabisa mchezo huo, pili unatakiwa kujua umeathirika vipi na mchezo huo.
Lazima ufike kwenye kituo cha afya na kuonana na mtaalamu ambaye atakuchukua kipimo cha ‘rectal examination’ ambacho kitaangalia umeathirika kwa kiwango gani.
Kama tatizo ni kubwa, unaweza kufanyiwa hata upasuaji au kama ni ndogo unaweza kupata tiba ya kawaida au ushauri, ikiwa ni pamoja na kuacha kabisa kuufanya mchezo huo.
Kama mtu ameathiriwa na mchezo huo na anapata shida kuuacha, anatakiwa apate tiba ya ushauri nasaha ambayo inaweza kumsaidia kuuacha, kisha kupata tiba kwa kuwaona wataalamu wa afya.
Wengi wamekimbilia katika kulegea misuli kwa kuhofia uzeeni wakati umri ukienda au wakati wa kujifungua na kusahau kuna maradhi ya hatari kama saratani ya eneo hilo (cancer of colon), ugonjwa wa UTI, yaani maambukizo kwa njia ya mkojo, tena huwa sugu, maana akitoa uume njia ya haja kubwa na kuuingiza sehemu ya kawaida, huingia na bakteria wanaoishi sehemu hiyo ambao wana madhara makubwa.
Kwa kifupi kama unaufanya mchezo huu unakikaribisha kifo au ulemavu. Kama umefanya kwa bahati mbaya au mazoea, unaweza kuwa huna madhara makubwa lakini kwa uhakika zaidi fika hospitali kwa uchunguzi na kupata tiba au utanitafuta na nitakuelekeza uende wapi.
GPL
No comments:
Post a Comment