Suleiman Kova
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
|
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema jana kuwa magari hayo, yalikamatwa katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Tabora.
Aliwataka watu ambao wamewahi kuibiwa magari kwenda kuyatambua na kutoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini kwani zipo kampuni feki zinazodai kujishughulisha na ukodishaji wa magari kwa bei za juu, kumbe hutumia mwanya huo kuyaiba. Wakati huo huo, Jeshi hilo limetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuwepo kwa wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeshika kasi kwenye taasisi mbalimbali za fedha.
Alisema linashirikiana kwa karibu na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na taasisi nyingine za fedha ili kudhibiti mianya ya wizi katika mashine hizo.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, hivi karibuni kuna wahalifu kutoka ndani na nje ya nchi ambao wametengeneza mtandao wa kuiba fedha kwenye mashine hizo kwa haraka na wapo waliowahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea.
“Mtu yeyote mwenye kadi ya ATM asitoe namba ya siri kwa mtu awe ndugu au rafiki kwa lengo la kufanya muamala, unapofika eneo la ATM asiombe msaada kwa mtu asiyemfahamu na kama kadi ina tatizo omba msaada kwa wafanyakazi wa benki husika, kariri namba na unapotaka kubadili fuata taratibu,” alisema Kova.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment