Vikosi vya Zimamoto wakizima moto kwenye moja ya majengo yaliyoko eneo la Ubungo(Millenium Busiss Park)juzi.Picha na Fidelis Felix
Dar es Salaam. Moto umeanza kuteketeza mabaki ya bidhaa zilizokuwa zimehifadhiwa katika maghala ya Ubungo Business Park Jijini Dar es Salaam
Moto huo ulianza Jumanne wiki hii ambao ulitokana na hitilafu ya umeme na kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha kutokana na kuteketeza bidhaa mbalimbali.
Magari zaidi ya 20 ya vikosi vya zimamoto na uokoaji vya taasisi mbalimbali ikiwamo Kampuni ya Ulinzi cha Knight Support (T) vilitumia zaidi ya saa 5 kuuzima bila mafanikio hadi jana majira ya saa 4.30 moto huo ulikuwa ukiendelea kuwaka.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Sunda (T) Limited, Mashaka Zuberi akizungumza na gazeti hili jana alisema ubunifu mdogo wa vikosi vya zimamoto umesababisha moto huo kuanza tena.
Alisema baada ya kutokea kwa moto huo (Jumanne wiki hii),vikosi vya taasisi mbalimbali vilijitokeza kuuzima na walipoona wamemaliza waliondoka.
“Moto huu bado unaendelea kuwaka na hii inatoikana na kutokuzimwa ipasavyo hivyo, hatujui hatima yake itakuaje kama utaendelea hivi hivi,”alisema Zuberi.
“Moto huu bado unaendelea kuwaka na hii inatoikana na kutokuzimwa ipasavyo hivyo, hatujui hatima yake itakuaje kama utaendelea hivi hivi,”alisema Zuberi.
Alisema kutokana na hitilafu hiyo ya umeme ambao umeteketeza bidhaa nyingi na kwamba wanafanya tathimini ili kubaini hasara waliyoipata.
Baadhi ya kampuni zilizokumbwa na janga hilo ni Sandu (T) Limited, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel, Hawk Security System,Poly Machinery na Brick Machinery.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment