Baadhi ya askari polisi wakisukuma gari lao lililoharibika katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam Machi mwaka huu . Picha na Maktaba.
Baadhi ya askari polisi wa chini wanaishi maisha magumu kutokana na kupata kipato kidogo huku wakiishi katika nyumba duni hali inayofanya utendaji wao kushuka
Baada ya shughuli nyingi za kutwa nzima, askari polisi Hashim (siyo jina lake halisi), anarejea nyumbani kujipumzisha.
Kwa kuwa nyumba anayoishi ipo umbali wa mita 700 kutoka katika kituo chake cha kazi, Hashim anaamua kutembea kwa miguu.
Kwa kuwa nyumba anayoishi ipo umbali wa mita 700 kutoka katika kituo chake cha kazi, Hashim anaamua kutembea kwa miguu.
Anafika nyumbani huku akitokwa jasho mwilini, lakini kabla ya kuingia ndani anawaza mengi, ikiwa ni pamoja na joto lililopo katika nyumba anayoishi na mke wake pamoja na watoto wao wawili.
Nyumba hiyo ni ya chumba kimoja na pia imeezekwa kwa mabati kuanzia juu mpaka chini.
Licha ya kukaribishwa kwa furaha na mkewe, Hashim anaingia ndani kwa unyonge, baada ya kubadili nguo za kazi anakwenda kuoga katika bafu la nje, ambalo hutumiwa na familia zaidi ya 20 za polisi wanaoishi katika nyumba za jeshi hilo (Kota) takriban 25 zilizopo Mtaa wa Mizengo (siyo jina halisi).

Wakati mwingine Hashim hulazimika kwenda katika nyumba ya wageni ili kumaliza faragha na mkewe kwa kuwa anaishi katika chumba kimoja, ana watoto ambao ni wakubwa na siyo jambo la busara kufanya tendo hilo huku wakishuhudia au hata kusikia kwa sababu katika kijumba hicho kidogo wanachoishi, hakuna faragha.
Acha tendo hilo, wakati mwingine hata anapokuwa akitaka kuvaa nguo, watoto ni lazima watoke nje, jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa.
Siyo Hashim pekee, wapo polisi wengi wanaoishi maisha ya aina hii katika mikoa mbalimbali nchini ambayo yanawafanya washindwe kutekeleza majukumu yao na wengine kuangukia katika vitendo vya kudai rushwa raia ili angalau wazibe mapengo.
Polisi wazungumza
Alipoulizwa kuhusu suala hilo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso alisema kwa ufupi, “Unasema wanalalamikia makazi wanayoishi kuwa ni duni…, sasa ingekuwa vyema kama ungetusaidia majina yao ili tuweze kuthibitisha malalamiko hayo.”

Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema vitendo vya rushwa kwa askari wa Jeshi la Polisi vinachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapato ya taifa hivyo kuifanya Serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake.

“Vitendo vya rushwa ni tabia ya askari mwenyewe na kama kuna askari wa juu anamwambia askari wa chini kumpelekea bahasha (rushwa) anatakiwa kutoa taarifa ili waweze kuchukuliwa hatua,” anasema Silima na kuongeza;
“Serikali haiwezi kuboresha mishahara huku wao wenyewe wanapunguza mapato ya taifa kutokana na vitendo vya rushwa, hivyo wanatakiwa kuachana na vitendo hivyo.”
Silima alikiri kuhusu nyumba za askari hao kuwa katika hali duni na kusema Serikali inajitahidi kuboresha makazi ya askari polisi.
Silima alikiri kuhusu nyumba za askari hao kuwa katika hali duni na kusema Serikali inajitahidi kuboresha makazi ya askari polisi.
“Ni kweli makazi ya askari bado ni tatizo, lakini hivi sasa kama unavyoona tumeshaanza kukabiliana nalo kule Kilwa (jijini Dar es Salaam) tumejenga na mikoani tunaendelea ili nao waishi katika makazi yaliyo bora,” anasema Silima.
Mkoa wa Dar es Salaam
Kwa wale wenye vyeo vya kuanzia meja kwenda juu, wao wako vizuri kidogo kwani hata makazi yao yako kwenye hali nzuri.
Hata hivyo, hali ni tofauti kabisa kwa wenye vyeo vya sajini kushuka chini. Kwani wao huishi katika mazingira magumu.

Mmoja wa askari hao kutoka Mkoa wa Ilala anasema kota moja (zilizopo eneo la Oysterbay) zina vyumba vitatu na hukaliwa na familia tatu, kwa watu wenye watoto inakuwa tabu kweli.
“Huwezi kuamini kota moja yenye vyumba vitatu, hukaliwa na familia tatu tofauti. Wakati mwingine inakuwa vigumu sana hasa mnapokuwa na watoto,” anasema.
Anasema wanachofanya ni kuwalaza watoto wa familia zote tatu katika ukumbi wa nyumba hizo, ili kuepuka kulala nao pamoja.

Namna ya kupata nyumba
Askari polisi mwingine kutoka Mkoa wa Kinondoni anasema mbali ya nyumba hizo kuwa ndogo ambazo hazistahili kuishi mtu mwenye familia, lakini hata kuzipata ni shida.
Askari polisi mwingine kutoka Mkoa wa Kinondoni anasema mbali ya nyumba hizo kuwa ndogo ambazo hazistahili kuishi mtu mwenye familia, lakini hata kuzipata ni shida.
Kwa kawaida askari polisi anapotoka chuoni, hufika kituoni akiwa yeye na mizigo yake michache. Kutokana na ukosefu wa maeneo ya malazi, hulazimika kulala kwenye mabwalo.
“Kwa kuwa mabwalo haya huwa ni makubwa, askari wa kike na wa kiume hutenganishwa kidogo tu saa nyingine kwa kutumia pazia, ilimradi wapate sehemu ya kujihifadhi,” anasema.
Anasema licha ya kuwapo kwa utaratibu maalumu wa kutafutiwa makazi, lakini ukweli ni kwamba suala la kuhama bwaloni hutegemea na ujanja wa askari husika.
Anasema licha ya kuwapo kwa utaratibu maalumu wa kutafutiwa makazi, lakini ukweli ni kwamba suala la kuhama bwaloni hutegemea na ujanja wa askari husika.
“Wapo ambao hupata vyumba kwa kulipia kwa askari wengine ambao wamejenga na wanakwenda kuishi uraiani.
Hivyo kutokana na kugharimia matengenezo mbalimbali katika makazi yao, askari hao hulazimika kuwalipisha fedha wale watakaohitaji vyumba,” anasisitiza.
Hivyo kutokana na kugharimia matengenezo mbalimbali katika makazi yao, askari hao hulazimika kuwalipisha fedha wale watakaohitaji vyumba,” anasisitiza.
Akizungumzia kwa upande wa vyoo anasema wakati mwingine hulazimika kutengeneza vyoo vya matairi, kutokana na ukweli kwamba vilivyopo vimejaa.
Mbeya
Baadhi ya polisi waliozungumza na gazeti hili jijini Mbeya kwa nyakati tofauti wanasema kuwa hali ya maisha yao ni mbaya, hasa kwa askari wasio na vyeo ambao ndiyo wanaoishi katika nyumba za polisi.
Baadhi ya polisi waliozungumza na gazeti hili jijini Mbeya kwa nyakati tofauti wanasema kuwa hali ya maisha yao ni mbaya, hasa kwa askari wasio na vyeo ambao ndiyo wanaoishi katika nyumba za polisi.
“Nyumba tunazoishi pale eneo la Sinde ni aibu, sisi wenye familia haifai hata kusimulia, kwani unapewa chumba kimoja cha kulala na sebule halafu una watoto unafikiri nini kinaendelea hapo,” anasema askari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Anasema mara nyingi wamekuwa wakiwalaza watoto sebuleni bila kujali jinsia zao, kwamba wakati mwingine ili wazazi wanapohitaji kukutana faragha huwalazimu kwenda kulala katika nyumba za wageni.
“Huwezi kufanya faragha na mkeo huku watoto wakiwa wamelala sebuleni halafu wa jinsia moja hivyo kwa sisi wengine tunaamua kuingia gharama nyingine ya kwenda kulala katika nyumba za wageni ili kuepuka kuwaharibu watoto kisaikolojia,” anasema.
Askari mwingine kwa sharti la kutotajwa jina anasema mazingira ya nyumba hizo ni machafu na kuna msongamano mkubwa wa watu hasa katika huduma ya choo kwani hutumiwa na watu wengi.
“Ukitaka kuona adha ya choo ni muda wa asubuhi ambapo kila mmoja anahitaji huduma ya bafu kwa ajili ya kuoga na kuwahi kazini, inakuwa kama sinema vile hivyo mazingira ya nyumba zetu bado hayafai,” anasema.
Kwa upande wake Koplo Atupele anasema kuwa kwa wale ambao ndiyo wanaanza kazi hupangiwa kulala kwenye bwalo ambapo hutandika magodoro chini, hulala eneo hilo mpaka watakapopata nafasi katika nyumba za serikali.
“Ndiyo maana utakuta askari wengine wanaamua kwenda kuishi uraiani ili kukwepa adha ambayo wanaipata kwenye kota,” anasema.
Itaendelea wiki ijayo
Mwananchi
No comments:
Post a Comment