IDDY MKWELA |
akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano huo wa raundi 6 kg,60 bondia wa siku nyingi ambae kwa sasa ni kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi
ambapo kutakuwa na mapambano mengi ya mchezo huo yatakayoanza saa kumi jioni ikiwa kiingilio ni miguu yako tu amewataka wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kuangalia mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira magumu
Nae Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Nassoro Mbwiga atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwela atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6
No comments:
Post a Comment