Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Zahanati ya Guluka Kwalala iliyopo katika Halmashauri yake baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpongeza Mkazi wa eneo hilo kwa kujifungua Salama mtoto wa Kwanza katika Wodi ya Wazazi aliyoijenga kwa nguvu zake kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni kutekeleza katika moja ya ahadi alizozitoa kwa wapiga kura wake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia na kumpongeza Bi. Halima Abubakari aliyejifungua mtoto wake katika Zahanati G/Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa amepakata mtoto wa Bi. Halima Abubakary mkazi wa Kata ya Gongo la Mboto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyejifungua salama usiku wa kuamkia Machi 19, 2013 kwenye Zahanati iliyojengwa na Mstahiki Meya ikiwa ni kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura wake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimchekesha mtoto huku akiwa ameshikilia zawadi ya mtoto kwanza kuzaliwa kwenye Zahanati yake.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika wodi ya wazazi iliyopo kwenye Zahanati ya G/Kwalala.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na makazi yao.
Tangazo la kutoa huduma ya kujifungua lililobandikwa nje ya Zahanati hiyo.
Bango la Zahanti ya Guluka Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Zahanati ya G/Kwalala imejengwa mwaka 2007-2010 na Mh. Jerry Silaa. Mwaka 2012 alijenga wodi ya kinamama kujifungua na kuaznia mwezi Februari 2013 iliwekwa vifaa vyote vinavyohitajika na aliahidi zawadi kwa mtiti wa kwanza ambaye amezaliwa usiku wa kuamkia tarehe 19 Machi, 2013.
6 comments:
zahati aliyoijenga yeye kwa wakazi wa eneo hilo.nijulisheni hii inamaana ni hela zake binafsi zimetumika ama ni nini. kama ni hela zake kuna tatizo hamezipata wapi?sidhani kipato chake halali kina muruhusu kujenga zahati.bongo siku hizi watu wanatoa fedha kwenye vyombo mbalimbali hata vya dini lakini ukijiuliza mikondo ya fedha hizo hujui imetoka wapi.Enzi za baba wa taifa watu walikuwa waoga kijianika hadharani.
Hata mimi anon March 20 najiuliza hivyo hivyo. Nafikiri ni Zahanati iliyojengwa na tax payers lakini labda imejengwa kipindi yeye alichokuwa meya hivyo waandishi wameandika ni Zahanati "Yake". Au anaweza kusema yeye ndio aliyeipigia kelele ikajengwa. Sidhani kama amejenga kwa fedha zange nafikiri aina hii ya uandishi inatupa shida sana walio wengi.
Na wewe nawe ..uliza tu swali kama amejenga kwa fedha zake au..hayo mambo ya Kambarage usituletee..we dont leave by past..kama walikua hawajianiki hadharani unamaanisha nao walikua wanachakachua halafu hawatangazi..si bora hao wanaojitangazia ni rahisi kuwakamata
Hamna hata wema binadamu kila kitu kazima mjenge hoja iwe hela zake au za ccm atajua mwenyewe tunacho hitaji huduma ya afya.Big up Jerry!!!
Kama ni za CCM au walipakozi sijui ila bora yeye aliyeamua kushea kidogo na aliowanyonya.
Ukiona mtu( hasa TZ) anajitangaza na vitu alivyofanya/toa kwenye jamii jua kuna nafasi fulani inaliwa ch
abo, inshort anatengeneza cv ya uchaguzi
Post a Comment