ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 13, 2013

NAIBU MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI AKUTANA NA KAMATI YA MAANDALIZI MISS UTALII TANZANIA TAIFA

Raisi wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo wa Kwanza Kushoto, Kaimu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Muheshimiwa Songolo pamoja na Ndugu Adam Chipungahelo, wakati walipofika katika ofisi yake.
Raisi wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akizungumza Jambo.
Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Muheshimiwa Songolo akiwa anafuatilia kwa umakini kikao.
Muheshimiwa Songolo Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni , akizungumza jambo.

Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania Ikiongozwa na Rais wa Mashindano hayo Ndugu Erasto G. Chipungahelo Jana Tarehe 12.03.2013 Ndugu..... katika ofisi yake iliyopo Kinondoni Manispaa Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Baadhi ya Viongozi wa Kamati hiyo ambaye ni Ndugu Adam Chipungahelo ambaye ni Mratibu wa Matukio Miss Utalii Tanzania na Bwana Fredy Njeje ambaye ni Meneja wa Masoko na mahusiano Miss Utalii Tanzania.

Ndugu Chipugahelo Alimshukuru Naibu Mustahiki Meya kwa mapokezi na ushirikiano wanayo pata kutoka kwa Manispaa hiyo ambapo warembo wapo kambini katika Hoteli ya Ikondolelo Lodge iliyopo Kibamba Manispaa ya Kinondoni. Amemuhakikishia Naibu Meya Kuwa Miss Utalii Tanzania Imejipanga kutangaza Utalii, Utamaduni na Mianya ya uwekezaji Manispaa ya Kinondoni kitaifa na Kimataifa ili hatimaye Kinondoni iwe kati ya Wilaya nchini.

Akizungumza katika Kikao Hicho Naibu Mustahiki Meya Aliwashukuru waandaaji wa Mashindano Hayo kwa Kuteuwa Manispaa ya Kinondoni kuwa makazi ya warembo wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13. Hii ni Fulsa pekee kwa Manispaa yetu kimataifa na Kimataifa lakini pia ni Fulsa kwa Manispaa ya Kinondoni kuuthibitishia Ulimwengu kuwa Tunavivutio vingi vya utalii kuanzia mahoteli, Maeneo ya kihistoria, Fukwe za Bahari na visiwa vya kuvutia vya Bahari, Aliwahakikishia waandaaji ushirikiano wa Hali na mali, ulinzi na ukarimu kwa wakati wote watakapo kuwepo kambini ndani ya Manispaa ya Kinondoni.

No comments: