ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 22, 2013

Nnko aliokoa mtu saa tatu mauti kumfika

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Koplo Eliza Nnko aliyeuawa katika ajali ya gari akiwa kazini na kuzikwa Dar es w Salaam, jana. Na Mpigapicha Wetu . 

Koplo Nko alizaliwa miaka 44 iliyopita Kijiji cha Ngarenanyuki, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha   
Dar es Salaam. Wakati askari Koplo Elikiza Nnko akizikwa jana,  imefahamika kuwa saa tatu kabla ya askari huyo kugongwa na gari na kusababisha kifo chake, aliokoa maisha ya mtembea kwa miguu, Joseph Msechu aliyegongwa na gari aina ya DCM.
Siku ya tukio, Msechu aligongwa na gari nyakati za saa 12:30 asubuhi eneo la Bamaga na Koplo Nnko alimwokoa kwa kumuwahisha Hospitali ya Mwananyamala na kuhakikisha anapatiwa matibabu. Msechu aligongwa na gari aina ya DCM eneo lilelile ambalo baada ya saa tatu kupita, Askari hyo alipata ajali iliyosababisha kifo chake.
Dada yake Msechu ambaye hakutaka kutajwa, alisema nusu saa kabla ya askari huyo kupata ajali, alimpigikia simu na kumuuliza hali ya kaka yake  na alimweleza jinsi alivyokuwa akiendelea.
Akizungumza kwa uchungu, mwanamke huyo alisema hakuamini alichosia kuhusu askari huyo kuwa amepoteza maisha eneo hilo hilo. Msechu kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), aligongwa na gari wakati akivuka barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwenda  ofisi za Startimes, baada ya kupata ajali hiyo, Koplo Nnko ndiye aliwapigia simu kuwafahamisha ndugu zake.
Alisema askari huyo ambaye alikuwapo eneo la tukio, alimwandikia marehemu fomu ya PF 3 na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na aliondoka baada ya kumkabidhi kwa ndugu zake walipofika huku akirejea kituo cha kazi.
Ajali hiyo ilimsababishia majeraha mdogo wake sehemu mbalimbali, ikiwamo kuvunjika mbavu mbili za upande wa kulia na moja upande wa kushoto na  kiuno.
Alisema baada ya kufika Muhimbili alipokelewa  na kufanyiwa vipimo zaidi na kwamba, hadi sasa amelazwa wodi namba 18  Jengo la Sewahaji. Hata hivyo, Mwandishi wa habari hizi alipofika Muhimbili alishindwa kuzungumz ana Msechu kutokana na wauguzi kumzuia.
Wakati huohuo,  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima na Mkuu wa Polisi nchini,  Said Mwema jana walioongoza mamia ya wananchi kwenye mazishi ya Koplo Nnko, aliyezikwa kwa heshima za kijeshi katika makuburi ya Mbweni, Manispaa ya Kinondoni.
Akitoa salamu za Serikali,  Silima alisema kifo cha askari huyo hakkikutokana na chanzo chochote zaidi ya dereva kutotii sheria za barabarani.
Mwananchi


No comments: