Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma |
Baadhi ya wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni imeiomba serikali kuruhusu mfumo wa analojia uendelea sambamba na wa digitali ili kutoa muda wa kutosha wa kutengeneza miundombinu.
Aidha, wamiliku hao kupitia Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) walisema kuwa kama muda iliotolewa kubadili mfumo ulikuwa haukutosha kujiandaa na matokeo yake ni kuwa wananchi wa kipato cha chini wanashindwa kupata haki ya kupata habari kutokana na kutomidi gharama za ving’amuzi. Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, alisema kuwa kwa kuwa uamuzi wa Tanzania kuondokana na mfumo wa analojia ulifanywa kwa mujibu wa sheria, utekelezaji wake utaendelea.
Alisema uamuzi wa kuiharakisha Tanzania kuingia katika mfumo wa digitali ni wa kujivunia na kwamba nchi kadha hivi sasa zinatuma watu wake kuja nchini kwa ajili ya kujifunza mfumo huo.
Profesa Nkoma alisema kuwa licha ya gharama za ving’amuzi kuwa kubwa, lakini wananchi wengi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuvinunua.
Alisema tangu mwaka 2005 mamlaka ilianza kufanya vikao na wadau kuhusiana na kubadili mfumo na kwamba walishirikishwa vya kutosha.
Alisema kufikia mwaka 2014 maeneo yote nchini yataanza kutumia mfumo wa digitali.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment