
PAPA mpya, Argentine Jorge Bargoglio ‘Papa Francis’ amehofiwa usalama wake kutokana na kuwa na tabia ya kujichanganya na watu tofautitofauti hivyo kuiweka roho yake mkononi.
Kwa mujibu wa mitandao, baada ya kuchaguliwa wiki iliyopita, Papa Francis aliamua kufuata vitu vyake alivyokuwa ameviacha katika hoteli moja iliyopo mjini Vatcan bila ulinzi wa kutosha, hali inayohatarisha usalama wake.
Kama hiyo haitoshi, kwenye ibada yake ya kwanza iliyofanyika Jumapili iliyopita ameonekana nje ya kanisa akishikana mikono na watu huku akibusiana na watoto wadogo pamoja na kuzunguka katika gari la wazi katika viwanja vya Mt. Peter mjini humo, vitendo ambavyo vilikuwa nadra kwa mapapa waliomtangulia.
Mapema wiki hii, papa alikutana na viongozi mbalimbali wa dini na wasiyo na dini kisha kuwaasa juu ya urafiki na upendo miongoni mwa wanadamu.
“Lazima tutetee na kuipenda amani ya dunia, tusameheane pindi tunapokoseana na tuwe wamoja,” alisema Papa Francis.
GPL
No comments:
Post a Comment