NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala amesema milango ipo wazi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kukutana na Serikali.
Serikali iko tayari kukaa na TFF kuzungumza nao ili kumaliza suala hilo na kumtaka rais wa shirikisho hilo kuacha upotoshaji kuhusu katiba yao.
Katiba iliyopo kwetu mpaka sasa ni ile ya mwaka 2006 na ndiyo maana tuliwaambia wafanye marekebisho kwa kutumia katiba hiyo yaliyofanywa hapo katikati na TFF iache kulumbana na serikali," alisema Makala
Kauli ya Makala imekuja ikiwa ni siku tatu baada ya Tenga kusema kuwa Waziri wala Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hawana nafasi ya kuingilia uchaguzi wao kwani TFF ni chama kamili kama vilivyo vyama vingine na kina uhuru wake wa kuamua mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa na Serikali.
Kuna wakati unaweza kudanganya watu, inafika mahali huwezi kudanganya tena katiba yao yenyewe ibara ya 1 (2) inasema TFF imesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya BMT ya mwaka 1967 na imefanyiwa marekebisho mwaka 1977. Kama inakiri wamesajiliwa kwa mujibu wa sheria iweje iseme serikali haina nafasi ya kuwaingilia.
"Chama cha mpira wa soka katika nchi yoyote ile kama hakijasajiliwa kwa kufuata sheria za nchi husika, Fifa haiwezi kutoa kibali kwa chama hicho kushiriki na kuendesha mashindani yoyote jambo ambalo hapa nchini linafanywa na BMT na Msajili ya Michezo nchini.
"Fifa inatambua Serikali bila ya muhuri wa Serikali hawezi kupata kibali sasa leo tumemnyima muhuri aseme hatuna nafasi, Tenga aache upotoshaji tena amemvunjia heshima mpaka Rais Kikwete kwa kuhoji uwezo wa Waziri ambaye amemteua.
"Nilimsikia Tenga akizungumza tena bila aibu anasema eti huyu mama hakuwa kwenye michezo anapotoshoshwa. Tenga anajua Waziri alipopitia mpaka Rais akamwamini na kumteua?"alihoji.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment