ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 5, 2013

BINGWA WA MASUMBWI NA BINGWA WA NGUMI NA MATEKE KUZIPIGA TANGA

Alan kamote mwenye rasta kulia
akimuadhibu mmoja wa mabondia aliowahi cheza nao
Bingwa wa kickboxing Hamis mwakinyo atazipiga na bingwa wa taifa wa ngumi za kulipwa nchini uzito wa light weight kg 60 Said mundi wa Tanga katika pambano la raundi nane, pambano la kusindikiza ubingwa wa mabara wa WBF kati ya Alan kamote na Jumanne Mohamed litakalopigwa katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga tarehe 17 mwezi huu.
Hamis mwakinyo ambae ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa WKN-AFRIKA(World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa dunia nchini iran anatazamiwa kuzipiga na Said mundi ambae ni bingwa wa ngumi wa taifa katika mpambano wenye ushindani mkali na unaozungumziwa na wapenzi wengi wa masumbwi mkoani Tanga. Kwa maelezo ya muandaaji wa pambano hilo promota ally mwanzoa anaeleza kuwa mabondia hao wamesharidhia makubaliano na wameshasaini makataba wa makubaliano wa pambano hilo. Akithibitisha hayo mbele ya Ibrahim kamwe kwa kumuonesha nakala za mikataba iliyosainiwa na mwanasheria wake,amesema pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa mabondia toka sehemu mbalimbali za Tanzania hususani Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu za majaji wa mchezo huo toka nje ya Tanzania ili kuondoa malalamiko yoyote yanayoweza jitokeza

No comments: