ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 10, 2013

Serikali yasaini mikataba kupeleka mawasiliano vijijini

Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa 

WIZARA ya Sayansi na Teknolojia kupitia mfuko wa kusimamia utoaji wa huduma ya Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF) imeingia mkataba na kampuni nne za simu za mkononi kwa lengo la kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata 52.
Katika mkataba huo, Serikali imetoa Dola 10 milioni kwa Kampuni  za Tigo, Airtel,Vodacom na TTCL, ili kufanikisha mkakati huo.
Akizungumza katika makubaliano hayo,Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alisema Watanzania wengi wanaoishi katika maeneo hayo wamekosa huduma za mawasiliano kutokana na changamoto ya kibiashara miongoni mwa kampuni hizo.
Makampuni haya hayako tayari kuwekeza huduma ya mawasiliano huko vijijini kwa sababu ya idadi ndogo ya watumiaji wa simu, ila kwa kutambua changamoto hiyo Serikali ikaamua kuanzisha mkakati wa kuhakikisha kuwa  huduma hiyo inawafikiaîalisema Profesa Mbarawa.
Alisema katika mfuko huo Serikali imepanga kutangaza zabuni nyingine ya kupeleka huduma hiyo katika kata 100 zilizoachwa katika kipindi hiki.
Serikali ilitangaza tenda ya kata 152 lakini zilizofanikiwa ni kata 52 tu, tulikuwa tumelenga idadi ya Watanzania 1.6 milioni waishio vijijini,îalisema Profesa Mbarawa.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga, alisema zaidi ya Watanzania 700,000 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.
ìSio hao tu ila tuna mpango wa kuwafikia Watanzania wote walioko vijijini, imekuwa ni changamoto sana, shughuli nyingi zinashindwa kufanikiwa kwa sababu ya ukosefu wa mawasiliano,îalisema Ulanga.
Kampuni hizo zitaanza kutekeleza mpango huo muda wowote kuanzia sasa baada ya kusaini kwa makubaliano hayo.
Kampuni ya Tigo imeingia mkataba wa kupeleka huduma hiyo katika vijiji 140 kwa gharama ya Dola za 1,402,150 wakati TTCL itafanya hivyo katika vijiji 119 kwa gharama ya Dola 2,130,698 ,milioni.
Vodacom iliyosaini mkataba wa Dola 102,900 kwa ajili ya kupeleka huduma katika  kata moja na Airtel itatoa huduma hiyo katika  kata 12 kwa gharama ya Dola 2,192,230.
Mwananchi


No comments: