Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema litaendelea kuagiza nguzo za umeme nje ya nchi kutokana na zile za viwanda vya ndani kutotosheleza mahitaji.
Mbali na kununua za nje, pia shirika hilo limesema litaendelea kununua za ndani zinazokidhi viwango vya ubora kulingana na makubaliano yaliyomo kwenye zabuni.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema Tanesco kama mashirika mengine ya serikali linafuata taratibu zote za manunuzi na kwamba hata linaponunua nguzo hizo kutoka nje, halikiuki sheria ya manunuzi.
Kampuni za ndani zilizoshinda zabuni ya kusambaza nguzo nchini ni Critical Engineering Solutions Construction Co, Sao Hill Industries Ltd na Mufindi Wood Poles.
Kampuni za nje ambazo ni kutoka Afrika Kusini zilizoshinda zabuni hiyo ni Treated Timbers Products, Low’s Treated Timbers (Ptg), Rousant International na Maghilika Timber Ptg Ltd.
Badra alisema kuwa Tanesco inatumia sheria ya manunuzi na kwamba kampuni zote zilishindanishwa kwa tenda na zilizoshinda zilitimiza vigezo ikiwa ni pamoja na bei elekezi.
Kwa mujibu wa Badra, kabla ya nguzo kupokelewa na Tanesco, hufanyiwa uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na majaribio ya kiufundi ili kuthibitisha ubora na kama zinakidhi viwango vya ubora vilivyoainishwa kwenye zabuni ndipo hati za kuzipokea zinasainiwa.
Alisema wazabuni wote wa ndani na nje hakuna hata mmoja ambaye nguzo zake zimewahi kukataliwa kwa kukosa ubora.
Kuhusu habari kuwa shirika hilo linalazimika kuagiza nguzo nje ya nchi kutokana na za ndani kukosa ubora, alisema si kweli kwani kila mzabuni aliyeshinda amekidhi viwango.
“Hadi sasa Tanesco ina mikataba inayoendelea na tutaendelea kupokea nguzo zinazozalishwa na kusambazwa kutoka katika viwanda vyetu vya ndani,” alisema.
Mwishoni mwa mwaka jana serikali ilipiga marufuku kwa shirika hilo kuagiza nguzo kutoka nje na badala yake inunue za hapa nchini pekee kwa lengo la kupunguza gharama.
Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, alipotembelea mkoani Iringa kikazi ambako alisema nguzo za umeme hazitaagizwa kutoka nje kutokana na viwanda vya ndani kukidhi viwango na na mahitaji.
Awali Meneja usimamizi wa magogo na mbao wa Kiwanda cha Sao Hill kilicho chini ya Taasisi ya Green Resource, alimweleza Simbachawene kwamba, kwa wakati huo wameshindwa kuzalisha nguzo hizo kwa vile wanakosa zabuni kutoka serikalini.
Wadau wengine wa nguzo hizo walimlalamikia Naibu Waziri kuwa tangu mwaka 2009 waliomba zabuni ya bidhaa hiyo Tanesco lakini wameshindwa kuzipata.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment