Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepinga vikali utaratibu uliotumiwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba waliodai kumpindua mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage.
Watu 607 waliojitambulisha kuwa ni wanachama wa Simba, waliitisha mkutano waliouita "Mkutano Mkuu wa Dharura" uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 17, 2013 na kukubaliana kuiengua Kamati ya Utendaji ya Simba chini ya Rage na kuunda kamati maalum ya kuisimamia timu yao katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa mkutano ulioitishwa na wanachama wa Simba na kisha kuuondoa uongozi wa klabu hiyo haukuwa halali kwa vile haukufuata taratibu na kwamba shirikisho hilo halitambui uongozi wowote ule wa kamati za muda kwa wanachama wake, zikiwamo klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Osiah alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana juzi jijini Dar Salaam chini ya mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa.
"Kamati imebaini kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 22(2) ya katiba ya Simba, Mkutano Mkuu wa Dharura huitishwa na Kamati ya Utendaji baada ya wanachama wasiopungua 500 kuwasilisha ombi hilo kwa maandishi na kujiorodhesha," alisema Osiah.
"Mkutano wa Machi 17 haukuitishwa na Kamati ya Utendaji ya Simba. Wanachama hao pia hawakufuata taratibu sahihi za kuiomba kamati ya utendaji ya Simba kuuitisha, waliandika barua kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo na kutupa nakala sisi (TFF) badala ya Kamati ya Utendaji ya Simba kama katiba ya Simba inavyotaka."
Osiah aliendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa katiba ya Simba, Kamati ya Utendaji ndiyo inayoitisha Mkutano Mkuu wa Dharura baada ya kuhakiki uhai na uhalali wa wanachama waliojiorodhesha kuomba mkutano huo na kwamba tayari uongozi wa Rage ulikuwa umeshawasilisha barua TFF ya kutotambua mkutano wa Machi 17 na pia maamuzi yoyote ya mkutano huo .
Aidha, Osiah alisema kuwa kamati ya Mgongolwa imesisitiza kuwa katiba za wanachama wote wa TFF hazina kipengele cha kura ya kutokuwa na imani na uongozi na ndiyo maana miaka kadhaa iliyopita wanachama wa Yanga, Chama cha Soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) na Chama cha Soka Mkoa wa Tabora (TAREFA) walipiga kura hiyo lakini TFF haikutambua uamuzi wao.
"Hata katiba ya Simba haitoi mamlaka kwa Mkutano Mkuu wa Dharura kufukuza uongozi uliochaguliwa. Katiba za wanachama wote wa TFF zimezingatia katiba za mfano za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambazo zinasema kiongozi ataingia madarakani kwa uchaguzi, na siyo kuteuliwa kwa mfumo huu wa kamati za muda," alisema zaidi Osiah.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment