Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu leo amefanya mkutano wa wanahabari. Katika mkutano huo, Lissu ameongea yafuatayo:
1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.
2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.
-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa
-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.
-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.
(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)
3 comments:
Ni jambo la kusikitisha kwa mtu kuandaa video ya kumkamatisha mtu kwa sababu tu ya ugomvi wa kisiasa.
Nimeangalia hiyo video inaonekana ni feki 100%. Inasikitisha kwa michuzi kuwasiliana na TISS kuwapongeza kuwa wamemuweza huyo Lwakatare...huko ni kukosa maadili ambayo ni dalili ya kutokuwa na malezi mema. Hivi kweli huyo Muhidini Michuzi ni mfanyakazi wa Ikulu? Kwa mtindo huu tutakuwa tunaendelea kwa kurudi nyuma wala hatutaenda mbele. Tumeona Ulimboka alikaribia kuuawa na hao hao wanaojiita usalama wa taifa hakuna aliyekamatwa hadi leo zaidi ya mwendawazimu aliyekuwa anaongea bila kujijua akisema pia alitumwa na Ikulu kumtesa Ulimboka. Jamani nchi yetu nzuri lakini kuna watu wanaiharibu wanadhani wanaisaidia serikali kumbe wanabomoa taifa letu lililojengwa imara na waasisi wetu.
Let's go to the basis, Was that recording occured? Did Lwakatare himself deny talking or being recorded sometimes, somewhere? If there is the action of calling someone you don't really know to talk or discuss anything of such magnitude, then He himself should first look into the inside of Chadema considering his position in Chadema. Romney did before Lwakatare and we know what happened to him in connection to past US election. Is mr. Lwakatare liked through his peers in Chadema? Only Chadema should tell the Tanzanian Mass.It is not only for Leaders in power to watch what they are talking and around who as the main ethic to leaders is to know and respect the country first,respect and hold life of any citizen, human as sacred regardless of personal perseption either politically or otherwise. Consequenses is the lesson. He should if found by court of law face it. Let's respect at least for this our Country, our people and the Law, Let's keep quiet and let the Law take it's course without influencing it through media. We have so many examples of ill justice in Tanzania because of such injustice procession through media.
POOR ARTICLE..... NEXT TIME USE SWAHILI
Post a Comment