ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 1, 2013

UNYAMA WA KUTISHA IRINGA: KIBAKA ACHOMWA MOTO; SAMAHANI KWA PICHA

Mwili wa kijana Paul Raphael Mtekele ukiwa umefunikwa baada ya kuteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba pampu ya kupulizia dawa mazao ya shilingi 25,000 katika kitongoji cha Tosamaganga B wilaya ya Iringa vijijini usiku wa leo(Tunaomba radhi kwa picha hizi)
Viatu vya marehemu vikiwa vimenusurika moto na mwili wake kuteketea kwa moto
Baba Mzazi wa kijana Paul mzee Raphael Mtekele ( wa tatu kushoto akiwa ameshika kiono )
Mzazi wa kijana huyo mzee Raphael Mtekele
Wananchi wa njia panda ya Tosamanganga wakilitazama gari la polisi ambalo lilikuwa limefika eneo la tukio. 

WANANCHI wanaosadfikika kuwa na hasira kali wakazi wa njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa wamemuua kwa kichapo mtuhumiwa wa wizi kijijini hapo Paul Raphael Mtekele na mwili wake kuuchoma moto baada ya kijana huyo kuvamia nyumba zaidi ya mbili kijijini hapo na kuiba mali mbali mbali ikiwemo pampu ya kunyunyuzia dawa mazao yenye thamani ya Tsh 25,000

Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kipanga B katika kijiji cha Njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa vijijini jimbo la Kalenga .
Kwa PICHA zaidi bofya  hapa Mzee wa Mtukio Daima

3 comments:

Anonymous said...

The suspect had been convicted, sentenced to death, and torched execution style by the supreme court of public opininion just because of Tsh. 25,000, equivalent to 16 US dollars. It is so sad that the value of human life matches exactly the cost of four heineken beers either at Seska Lounge or Swahili Village. Qustions to kellers; how do you feel now down deep in your hearts??? Have you ever comitted and got away with any crime since you were born??? Why him and not yourselves???

Anonymous said...

Nimekuwa nikiona haya mambo mara kwa mara,inasikitisha sana baba yake yuko pichani fikiria kama angekuwa ndugu yako.Naomba atayesoma aongee ili hawa watu wenye fikira ndogo waache haya mambo ya kinyama.

Anonymous said...

Tanzania and Africa in general will never progress, until we appreciate human life. That is a fact, and there is no way around it. I think someone should translate this to Swahili.