Mjumbe wa Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kufuatilia kufeli kwa Wanafunzi wa Darasa la 12 wa mwaka 2012 Nd. Mabrouk Jabu Makame akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Wajumbe hao ambao wanaendelea kufuatilia suala hilo katika Mikoa yote ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baadhi yao huvu sasa wanaendelea na kazi hiyo katika mikoa ya Zanzibar
Mjumbe wa kufuatilia kufeli kwa wanafunzi wa darasa la 12 wa mwaka 2012 Bw. MohdMringo akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambapo yeye na baadhi ya wajumbe wenzake wanaendelea na jukumu lao katika Mikoa mbali mbali ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wa darasa la 12 la mwaka 2012. Aliwataka wajumbe hao kufanya utafiti wa kina utakaosaidia kuibua njia ya kuepuka kasoro zinazotoa mwanya wa kufanya vibaya wanafunzi hapa Nchini.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment