Wakurya na familia zao wanaoishi Marekani wanatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza Maryland nchini Marekani kuendeleza mila na desturi ya kabila lao na kitu muhimu kuwaonyesha watoto wao wapi walikotoka.
Akiongea na Vijimambo Wambura amesema hii shughuli ni muhimu sana kwa Wakurya waishio Marekani kuifikiria na kupanga safari ya kuja Maryland ili kuifanikisha. lengo kubwa ni kukutana, kujuana na pia watoto wetu waweze kujua wapi tulikotoka na tutakua na nyama choma, kichuri,kucheza litungu na kuibhaka.
Address itakayofanyikia ni
6063 Joseph Scott Drive,
Elkridge, MD 21075
Siku ya Jumamosi May 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana (12 noon)
Siku ya Jumamosi May 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana (12 noon)
KARIBUNI SANA
9 comments:
Rejea hotuba ya Baba wa Taifa,1995 Dodoma,iko kwenye utube. Alisema kuendekeza ukabila hakuna la manufaa zaidi ya kufanya matambiko.
Nyerere must be turning in his grave! Wachagga wakikutana maneno? Ama wakurya wa Kenya hawa?
Tulianza na Jumuiya ya watanzania DMV. Tukaendelea hadi tukafungua matawi ya vyama vya siasa (CCM na CHADEMA) na sasa hivi tunaenda kwenye ukabila. Kilianza kikao cha Wahaya ambacho kwa kauli moja walikubaliana kuanzisha chama chao na michango ya $ 50 kama entrance fee. Leo Wakuria nao wameamua kuzinduka kutoka usingizini. Nini kitafuata siku zijazo? Stay tuned.
Na wewe anzisha cha kabila lako au huna kabila?
duuuu jamani kwa nilivyoelewa mimi ni kwamba hawa wanataka wakutane wale wachome,wacheze kikwao na sio kuanzisha cha kikabila, mie mwenyewe natamani ningepata mtu wa kabila langu angalau tuongee kikwetu au tule chakula cha kikwetu, Dj labda ungeongeza kwa kusema na wengine mnakaribishwa. Tujaribu kusoma vizuri na kuelewa maana. Tuache chuki binafsi
Mukore bhuya abhaghaka!!
wajameni,sio vibaya watu wa utamaduni mmoja wakikutana kubadilishana mawazo. mwisho wa siku wote ni watanzania,ni vizuri kuungana mkono watu wanapojaribu kukutana pamoja.kaka wambura,hongera kwa juhudi nzuri za kukutanisha watu wa mila moja.
Haya majibizano yanahusisha wasomi watupu. Hapo ndipo utakapojua ubora wa elimu yetu.
Jamani this is a joke! This is 2013 hivi kiswahili is not enough kutrufurahisha kama WATANZANIA???? DMV KUNA MAMBO?????
Post a Comment