ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 27, 2013

WANANCHI WAELIMISHWE KWA LUGHA ZAO



Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakijadiliana moja ya mada iliyohusu matumizi ya lugha katika kutoa elimu kwa jamii, katika masuala mazima ya kuilemisha na kuifahamisha jamii mambo mbali yakiwemo ya kimaendeleo,Warsha hiyo ilifanyika kwa kwa hisani kubwa ya kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Fedha na Wanahabri wengine wakiwemo wa mitandao ya kijamii, ambapo mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida ilikuwa ikijadiliwa.

Mwenyekiti wa mjadala huo. Bw. Josephat Lukaza ambae ni mmiliki wa Likaza Blog akichangia hoja mbele ya baadhi ya wamiliki wa wamiliki wa mitandao ya kijamii.

Kufuatia lugha kuwa kikwazo kikubwa cha kufikisha ujumbe kwa baadhi ya jamii nchini, imeshauriwa kwamba baadhi ya jamii zenye misimamo ya kitamaduni, zifikishiwe taarifa mbali mbali za kimaendeleo kwa kugha zao ili ujumbe huo upate kueleweka.


Uchunguzi uliofanyika hivi karibuni na baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii, umegundua kwamba imekuwa vigumu kwa wananchi wa kawaida kuelewa taarifa mbali mbali za kimaendeleo kutokana na lugha wasilishi, ambapo taarifa nyingi zimekuwa zikiandikwa kwa lugha za kigeni jambo ambalo huwa ni kikwazo kikubwa kwa wananchi wa kawaida kuzielewa.


Hoja hii iliibuka wakati wa kujadili jinsi ya kufikisha taarifa za kimaendeleo kwa wananchi wa kawaida, katika warsha iliyoandaliwa na wizara ya fedha na kuhusisha wamiliki wa Magazeti tando, ambapo mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida ilikuwa ikijadiliwa.


"Wengi wa wananchi, hawa wa vijijini si wataalam wa lugha kwa mfano za kiingereza, hivyo wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa wanachotaarifiwa na hivyo kubaki kuwa hawajui chochote kinachoendelea katika nchi", alisema wakati akichangia mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, bwana John Bukuku.


Moja kati ya jamii zinazopata taabu katika kupokea taarifa hizi huwa ni kwa mfano wamasai. Hawa wamekuwa wakizungumza lugha yao tu wanapokuwa majumbani mwao na si wengi ambao wamebahatika kwenda kujifunza lugha za kigeni kwani jamii hii imetawaliwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ufugaji.
Maofisa habari toka sekta mbali mbali nchini Tanzania wakiwa katika majadiliano.


Katika Warsha hiyo ya siku ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa habari (pichani) kutoka sekta mbali mbali za kimaendeleo, wadau walikuwa wakitafuta njia mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea.


Akichangia, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya fedha, Bi Ingiahedi Mduma, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya fedha, ipo haja ya kuwa wabunifu katika kuhakikisha kwamba kwa njia yoyote ile, tunahakikisha kwamba wananchi wa kawaida, hasa wa vijijini, wanapata taarifa husika kwa wakati muafaka.


Amesema taarifa za kimaendeleo za nchi ni haki ya kila mwananchi kujua na ndio maana sasa wameamua kukaa chini na kuumiza kichwa katika kutaka kujua jinsi ya kuwafikia asilimia kubwa ya wananchi, mijini na vijijini.


Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro Park, maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani ambapo pia mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ilijadiliwa.

Habari na picha kwa hisani ya Cathbert Kajuna, Kajunason Blog

No comments: