ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 23, 2013

Wasanii kupamba Uapisho kenya

Timu ya taasisi ya rais mteule Uhuru Kenyatta kwa sasa inashughulikia orodha ya wasanii watakaofanya onyesho kubwa kabisa katika siku ya kuapishwa kwa mheshimiwa huyu, na inatajwa kuwa wasanii hawa watakuwa ni kutoka Marekani, Jamaica, Nigeria, Ghana, Afrika Kusini pamoja na Tanzania.
Baadhi ya majina ambayo mtandao mmoja maarufu umeyaweka wazi, ambao watafanya mazungumzo na timu hii kuangalia uwezekano wa kuhudhuria na kutumbuiza katika siku hii ni pamoja na Rihanna, Chris Brown, Nicki Minaj, Toni Braxton, pia Alaine na Burning Spear kutoka Jamaica.
 Maandalizi ya onyesho hili kubwa kabisa kwa sasa yapo katika hatua za awali, na kwa taarifa tu ni kwamba, tukio la wasanii hao litakuwa ni tofauti na sherehe rasmi za kiserikali za kuapishwa kwa rais huyo

No comments: