Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza kuanza uchunguzi dhidi ya watu waliopoteza hati za kusafiria baada ya kubainika kuwa baadhi ya watu wamezigeuza kuwa biashara kwa kuziuza kwa watu ambao siyo raia wa Tanzania.
Naibu Waziri wa wizara hiyo ,Pereira Silima, alisema hayo jana wakati akihojiwa na Redio One katika kipindi cha Kumepambazuka kuhusu kuzagaa kwa hati za kusafiria zinazotumiwa na watu ambao siyo Watanzania.
“Kumekuwapo na ongezeko la matangazo ya kupotea kwa hati za kusafiria pengine inawezekana baadhi wanaamua kuziuza kwa watu ambao siyo Watanzania, kwa hiyo tutafanya uchunguzi na tukibaini tutachukua hatua dhidi ya waliouza hati zao kwa wasio Watanzania,” alisema Silima.
Alisema Watanzania wanaouza hati zao lazima wafahamu kuwa wanafanya kosa na kwamba katika uchunguzi huo watawasiliana na ubalozi wa China ambako suala la watu wasio watanzania kutumia hati za kusafiria limelipotiwa.
Silima alisema baada ya kupata taarifa hizo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepata wasiwasi kwamba watu ambao mara kwa mara wamekuwa wakitangaza katika vyombo vya habari kupotelewa hati za kusafiria huenda baadhi yao wasio waaminifu wamekuwa wakiziuza kwa watu ambao siyo Watanzania.
Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilitangaza kushtukia kuibuka kwa biashara ya ununuzi wa hati za kusafiria za Tanzania inayofanywa na watu wasio Watanzania.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Huduma, Abbas Irovya, alisema kutokana na hali hiyo, kwa mwaka hati zinazopotea kwa wastani ni 360 na hakuna taarifa za kurejeshwa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment