Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela , alisema jana kuwa msako huo ulilenga kuwakamata wezi na wahalibifu wa miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kinondoni.
Alisema katika msako huo uliosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, ulifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wakiwa na pampu 86 za kusukumia maji, mita za kusoma maji 19, matenka ya malori yaliyojazwa maji kwa njia ya wizi 11.
Kenyela aliongeza kuwa watuhumiwa wote wameshafunguliwa mashitaka katika vituo mbalimbali vya polisi na baadhi yao kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.
Alisema kupitia operesheni hiyo, tayari baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Kinondoni yameanza kupata maji, ambayo ni Magomeni Makuti, Mwananyamala na Mikocheni.
Alisema msako huo ulihusisha maeneo ya Mbezi kwa Musuguri, Mbezi Luis, Magomeni, Kinondoni, Mwananyamala, Kimara, Kibamba, Msasani, Namanga, Kijitonyama, Mwenge, Mikocheni na Mabibo.
Aidha, Kamanda Kenyela alitolea ufafanuzi mpango wa wananchi wa Jimbo la Ubungo wakiongozwa na Mbunge wao, John Mnyika (Chadema) kutaka kuandamana kuelekea ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (Dawasco) Jumapili ijayo kudai maji katika jimbo hilo na kusema suala hilo litatolewa ufafanuzi leo baada ya kukutana na viongozi wa Chadema na kukubaliana.
Hivi karibuni, Sadiki akiambatana na Rugimbana pamoja na Jeshi la Polisi na kuendesha msako wa kuwakamata watu wanaolihujumu Dawasco kwa kujiunganishia maji kiholela.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment