ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 7, 2013

YATIMA MWENYE MIAKA 15 AZIDI KUFANYA VIZURI CHUO KIKUU CHA ZIMBABWE

Maud Chifamba (15) akiwa Chuo Kikuu cha Zimbabwe anaposoma Shahada ya Uhasibu.
Maud (wa pili kushoto) akipokea msaada wa Laptop kutoka kwa wafadhili.
Maud akipokea mfano wa hundi kwa ajili ya masomo yake chuoni kutoka Mamlaka ya Mapato Zimbabwe (ZIMRA).
(Picha kwa hisani ya Mamlaka ya Mapato Zimbabwe (ZIMRA))

Clarence Mulisa wa GPL na Mitandao
-ALIVUSHWA KUTOKA DARASA LA 3 MPAKA LA 6
-ALISOMA ELIMU YA KIDATO CHA 4 KWA MIAKA 2 AKIWA NYUMBANI NA KUFAULU VIZURI
-ALIJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 14 MWAKA JANA
MWANACHUO mwenye uwezo wa kipekee anayesoma katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Maud Chifamba (15), amezidi kufanya maajabu katika mitihani yake ya kwanza akiwa chuoni hapo. Maud ambaye amevunja rekodi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe kwa kujiunga akiwa na umri wa miaka 14 mwaka jana akisomea Shahada ya Uhasibu, amefaulu kwa kiwango cha juu zaidi ya wenzake hasa katika masomo mawili.

Maud aliyepata alama 12 katika mitihani yake ya kidato cha sita baada ya kumaliza elimu ya sekondari ndani ya miaka miwili akiwa nyumbani, alitangazwa na Jarida la Forbes kuwa mmoja wa wanawake mahiri barani Afrika akiwa na umri mdogo huo.

Maud anasema "Nina furaha kusoma katika chuo hiki maana wanachuo wote wa kiume na wa kike wananijali na wananichukulia kama mdogo wao pia wananisaidia pale ninapohitaji msaada wao
Ninajisomea wakati wa usiku na kitu kinachojitia nguvu zaidi na kunifanya niongeze bidii ni mazingira niliyotokea. Ninajituma kwa ajili yangu pamoja na kaka zangu" alisema Maud.
Maud ana ndoto za kuwa mfano wa kuigwa katika ulimwengu wa biashara ambapo ana matumaini ya kuwa na kampuni yake siku moja.

Maud alizaliwa Novemba 19, 1997 katika familia ya wawindaji eneo la Chegutu. Baba yake mzazi alifariki akiwa na miaka mitano na kulelewa na mama yake ambaye naye alifariki mwaka 2011.
Kutokana na kipaji chake katika masomo, alipandishwa madarasa kutoka darasa la tatu mpaka la sita. Alimaliza elimu yake ya msingi akiwa na miaka tisa na kufaulu vizuri katika masomo yake yote.

Kutokana na matatizo ya kifedha, alishindwa kuendelea na masomo ya sekondari, hivyo kuamua kujisomea akiwa nyumbani. Alihitimu kidato cha nne ndani ya miaka miwili na kufaulu vizuri kwenda kidato cha tano na sita.

Kipaji chake cha kipekee kimemuwezesha kupata wafadhili kutoka makampuni tofauti ambapo anaufadhili wa miaka minne kwa masomo yake chuoni kutoka Mamlaka ya Mapato Zimbabwe (ZIMRA).

Mshauri wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, bwana Munyaradzi Madambi, anamuelezea Maud kama binti mtulivu.
Tunayo furaha kuwa na binti huyu mwenye kipaji cha pekee. Tunafarijika sana nae maana nimkarimu na mnyenyekevu si kwetu tu bali kwa kila mtu hapa chuoni." Alisema bwana Munyaradzi.

CHANZO: www.zimeye.org

No comments: