ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 16, 2013

ZITTO AMGALAGAZA CHEYO

Zitto Kabwe,

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, jana aliibuka kidedea katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Hesabu za Serikali na kumbwaga aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).
John Cheyo

Uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa kamati hiyo ulikuwa wa vuta nikuvute kati ya Zitto na Cheyo ambapo awali ilidaiwa kuwa kamati hiyo ilivunjwa na Spika ili kupunguza nguvu ya CHADEMA bungeni.

Hata hivyo kampeni za wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ziliendelea kufanyika hadi jana ambapo wabunge hao walitaka kumuangusha Zitto ili chama hicho kikuu cha upinzani bungeni kisiwe hata na mwenyekiti mmoja.

Katika kuunda kamati za Bunge kulikuwa na mabadiliko ambapo baadhi ya kamati ziliongezwa na nyingine kuvunjwa huku Spika wa Bunge Anna Makinda akieleza kuwa ni mfumo wa mabunge mengine kutoka katika nchi nyingine.

Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema kwa mujibu wa taratibu za Bunge, Spika alimchagua Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, huku kaimu akitakiwa kuchaguliwa na wabunge ndani ya kamati.

Hata hivyo katika uchaguzi huo kaimu mwenyekiti hakuweza kupatikana kutokana na idadi ya wabunge kuwa ndogo na kwamba atachaguliwa siku ya Jumatatu.

Wenyeviti wengine waliochaguliwa katika kamati mbalimbali ni pamoja na Fedha na Uchumi Mahmoud Mgimwa ambapo Makamu wake ni Luke Kitandula.

Kamati ya Bajeti Mwenyekiti ni Andrew Chenge, Makamu ahajachaguliwa; na Hesabu za Serikali (PAC) Mwenyekiti ni Zitto Kabwe na Makamu ni Deo Filikunjombe.

Serikali za mitaa (LAAC) Mwenyekiti Rajab Mbarouk Mohammed na Makamu ni Suleiman Jummanne Zed.

Huduma za Jamii Mwenyekiti ni Margreth Sitta na Makamu ni Stephen Ngonyani, huku Maendeleo ya Jamii Mwenyekiti ni Jenista Mhagama na Makamu Saidi Mtanda.

Kamati ya Nishati na Madini Mwenyekiti ni Victor Mwambalaswa na Makamu ni Jerome Bwanausi.

Ardhi, Maliasili na Mazingira Mwenyekiti ni James Lembeli na Makamu wake ni Abdulkarim Shah. Miundombinu Mwenyekiti ni Peter Serukamba na Makamu wake Juma Kapuya.

Kamati nyingine ni Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mwenyekiti ni Hamis Kigwangalla na Makamu ni John Lwanji. Kamati ya Masuala ya Ukimwi Mwenyekiti ni Lediana Mng’ong’o na Makamu wake ni Diana Chilolo.

Ulinzi na Usalama Mwenyekiti ni Anna Abdallah na Makamu ni Mohamed Seif Khatib.

Mambo ya Nje Mwenyekiti ni Edward Lowassa na Makamu ni Mussa Zungu. Katiba, Sheria na Utawala Mwenyekiti ni Pindi Chana na Makamu ni William Ngeleja.

Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Mwenyekiti ni Hassan Ngwilizi na Makamu ni John Chiligati. Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Mwenyekiti ni Prof. Peter Msolwa na Makamu ni Saidi Nkumba.

Chanzo: http://www.freemedia.co.tz

No comments: