Sunday, March 31, 2013

ZOEZI LA UKOAJI BADO LINAENDELEA, WATU 26 WAMEFARIKI DUNIA

Takribani watu 26 wamethibitishwa kufariki mpaka sasa baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka katikati ya Dar es Salaam Ijumaa ya Machi 28, 2013.
Akidhibitisha Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Seleiman Kova alisema mpaka sasa wameshatoa watu wapatao 43, ambapo 24 wamefariki na 17 majeruhi. Ambapo inasadikika watu wapatao 60 walifunikwa na jengo hilo.
Alisema kwa sasa hakuna upungufu wowote wa vifaa, Hakuna upungufu wowote maana wataalam toka JWTZ, Ubalozi wa China. Vile vile watu mbali mbali wamejitolea magari, vijiko kuhakikisha zoezi la uokoaji liende kwa kasi zaidi.
Aliongeza kuwa changamoto ni kuhakikisha mtu yeyote aliyefukiwa katika kifusi aweze kupatikana.
Jeshi la Polisi limemkamata watu watano akiwemo Bw. Ally Razack ambaye ni mmiliki wa jengo ambapo kibali kilikuwa kinaonyesha alitakiwa kujenga ghorofa 9 ila yeye alijenga zikafika ghorofa 16, mkandarasi na viongozi watatu wa Manispaa ya Ilala ya jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 na kuua watu 26 wengine 17 kujeruhiwa vibaya ingawa mpaka sasa maiti bado zinaendelea kupatikana na kusababisha idadi kamili ya maiti zilizopatikana kutokuwa kamili.
Ukiangalia kwa makini picha hii, utaona mguu wa mtu aliyekuwa amefunikwa na kifusi.
Waokoaji wakijitahidi kutoa mwili wa mtu aliyekuwa amefunikwa na kifusi.
kwa picha zaidi bofya read more
Hali ya uokoaji bado ikiendelea kwa kasi.
Wakiangaika kuokoa mtu aliyekuwa amefunikwa na kifusi.
Heka heka za uokoaji zikiendelea.

 KAJUNASON BLOG

1 comment:

Anonymous said...

The price of corruption. This kind of accidents will be a continuous never ending thing until we make real changes. We are a reactive nation so far. I fell like we are not protected.

God bless Tanzania!