Katavi. Polisi Mkoa wa Katavi inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Majimoto, wilayani Mpanda kwa tuhuma za kuwaua watoto wake watatu kisha kuwatumbukiza kwenye kisima cha maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhairi Kidavashari alisema tukio lilitokea juzi saa 11:00 alfajiri baada ya kuibuka ugomvi mkubwa kati ya mkazi huyo na mkewe, Jacquline Lukevi (21) ambaye alinusurika kifo baada ya kutumbukizwa kisimani, lakini hali yake ni mbaya.
Kidavashari aliwataja watoto waliouawa kuwa ni ni Maria (miezi 4), Eliza (4) na Frank (6).
Kidavashari aliwataja watoto waliouawa kuwa ni ni Maria (miezi 4), Eliza (4) na Frank (6).
Alisema chanzo cha mauaji hayo, ni ugomvi wa wanandoa hao baada ya mwanaume kudhani mkewe ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine, kitu ambacho kilikuwa kikisababisha ugomvi mara kwa mara kati yao.
Habari zinadai kuwa, baada ya kuibuka kwa ugomvi huo kijana huyo alianza kupiga watoto wake na mama yao kwa silaha mbalimbali, akiamini tayari amewaua wote alianza kuwaburuza hadi nyumbani kwa Kawaida Jonas ambako kuna kisima cha maji na kuwatumbukiza.
Hata hivyo, wakati akifanya kitendo hicho aliudondosha mwili wa Maria barabarani, baadaye baadhi ya wananchi waliuona na kwenda nyumbani kwake na kmuuliza kuhusu mauaji ya mtoto huyo.
Inadaiwa kijana huyo alitoa majibu yenye utata kwamba, watoto wote wameondoka na mama yao mzazi.
Inadaiwa kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi hao walimwacha mtuhumiwa na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Majimoto, ambao walifika eneo la tukio na kuanza kufuatilia na kubaini miili walikuwa imetumbukizwa kwenye kisimani nyumbani kwa Jonas.
Baada ya kubaini hivyo, askari waliopoa miili hiyo huku watoto wawili wakiwa wamefariki, lakini mama yao akiwa hai, bali alikuwa hawezi kuongea.
Kidavashari alisema mwanamke huyo alikimbizwa Kituo cha Afya Mamba kwa matibabu, ingawa hali yake inaeelezwa ni mbaya.Alisema mtuhumiwa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment