ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 2, 2013

CCM Afrika Kusini yamsaka katibu wake kwa tuhuma za kuwatapeli Watanzania

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Afrika Kusini inamsaka aliyekuwa katibu wake, (jina linahifadhiwa), ili kimfikisha katika vyombo vya kisheria, kutokana na tuhuma za utapeli.
Anatuhumiwa kuwatapeli baadhi ya Watanzania waishio Afrika Kusini, Rand 200,000, zaidi ya Sh37 milioni, kwa kutumia kampuni iliyosajiliwa kwa jina la mkewe, ya masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano.
Anadaiwa kuwa alifanikiwa kuwatapeli Watanzania hao kiasi hicho cha pesa kwa mtindo wa upatu, baada ya kuwashawishi wawekeze pesa zao katika kampuni hiyo na kwamba baada ya muda wangepata faida.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alifanikiwa kuwashawishi Watanzania hao kuwekeza pesa zao katika kampuni hiyo akidai kuwa ilikuwa inashughuli za biashara ya (Forex & Stock Marketing), lakini baada ya Watanzania hao kuwekeza, alikimbia nazo bila kuwalipa.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Afrika Kusini, Kelvin Nyamori alilithibitishia Mwananchi na kusema kuwa kutokana na tuhuma hizo aliitisha kikao cha dharura cha Sekretarieti na kumvua wadhifa wake huo na kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali vikiwamo vyombo vya kisheria.
“Kamati, tulishafanya kikao cha dharura kumsimamisha kazi yake ya ukatibu, baada ya kupata tarifa hizo, kutokana na malalamiko ya waliodhulumiwa,” alisema Nyamori na kuongeza:
“Tumeshatoa taarifa Ubalozini na kituo cha polisi. Tunamtafuta mtuhumiwa ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria, kwa kufanya utapeli kwa kutumia jina la chama kimya kimya.
Alitoa wito kwa mtu yeyote Tanzania anayemfahamu, atakapomuona au kama anajua mahali aliko, atoe ushirikiano kwa kuwasiliana na CCM Afrika Kusini.    
Mwananchi 

2 comments:

Anonymous said...

CCM DMV, mnasikia hayo atakwenda JELA mtu au watu hapa , clock is ticking tik

Anonymous said...

CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!