Watoto wa darasa la lugha ya kiswahili wakiwa darasani wakisaidiwa na walimu wao leo Jumamosi April 20, 2013 College Park.
Wanafunzi wa darasa la lugha ya kiswahili wakifuatilia jambo kutoka kwa mwalimu wao kwenye darasa hilo lililokua likiedelea leo College Park, Maryland leo.
Watoto wa darasa la kiswahili wakifuatilia mafundisho ya darasa la kiswahili College Park leo Jumamosi.
Wanafunzi wakiwa darasani.
Mwalimu akifundisha kwenye darasa la lugha ya kiswahili College Park leo Jumamosi April 20, 2013.
Juu na chini mwalimu na watoto wanaojifunza kiswahili wakiwa darasani
3 comments:
Hongera sana wana-DMV kwa kubuni na kuanzisha programu hii ya kuwafundisha watoto wa Kitanzania lugha ya Kiswahili. Pamoja na kuwawezesha kujivunia utambulisho wa asili yao, hawa ndio wataja kuwa wataalamu wa Kiswahili wa kesho na hivyo kufanya taaluma za isimu ya Kiswahili, fasihi ya Kiswahili na ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni kuwa endelevu. Endelea na jitihada zenu.
Hawa wafundishaji wanastahili sifa sana. Kazi nzuri kwa kweli...
kazi nzuri sana mnaifanya jamani nakupeni heko lakini wajuwe kutamka vizuri pia kwa lafzi ya kifasaa ya kimwambao ndo kiswahili kilipotoka na kuchipukia jamani wafundisheni wajue kukisema kwa ufasaha
Post a Comment