Picha juu na chini ni katika pita pita ya Vijimambo Kijitonyama, Dar es Salaam, ikakutana na ghorofa limeanguka na ilipouliza ikaambiwa lilianguka miaka minne iliyopita Na kuanguka kule kulisababisha kifo cha mtoto wa familia ambayo ilikuwa inaishi ndani ya ghorofa hilo. Mwenye hilo ghorofa alishakufa, watoto wake wameshndwa kuendeleza marekebisho ya hilo ghorofa kwa sababu za kiuchumi. La kushangaza ni kwamba, pamoja na kuwa lilianguka miaka mingi iliyopita, mamlaka haijachukua hatua za kiusalama kuondoa mabaki ya vifusi ambayo yanaweza hatarisha usalama wa nyumba za jirani na maisha yao. na kuwa maficho ya vibaka.
No comments:
Post a Comment