ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

Kesi dhidi ya Lwakatare kutajwa leo

Wilfred Lwakatare
Ni ya tuhuma za ugaidi inayomkabili mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chadema, Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Chadema,  Joseph Ludovick, lipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es salaam,hivi karibuni.

 Machi 20 mwaka huu, Wakili wa Serikali, Prudence Rweyongeza alidai kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo kinyume cha kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo inatarajia kuitaja kesi inayomkabili Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezahura wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi.Kesi hiyo, inatarajiwa kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, ili kutoa nafasi ya kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.Katika kesi hiyo, yenye mashtaka manne ya ugaidi, Lwakatare na Joseph, pia wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.
Machi 20 mwaka huu, Wakili wa Serikali, Prudence Rweyongeza alidai kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo kinyume cha kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28 mwaka jana katika eneo la King’ong’o, wilayani Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walikula njama ya kumdhuru kwa sumu, Msacky ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.

Katika kesi hiyo, Lwakatare anatetewa na mawakili watano ambao ni, Peter Kibatara, Mabere Marando, Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na Tundu Lissu.

Wakati huohuo, maombi ya Lwakatare kupinga utaratibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka kumfutia mashtaka kisha kumkamata na kumfungulia mengine, yameiva kwa kupangiwa tarehe ya kuyasikiliza.

Habari zilizopatikana jana kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, zilisema maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Lawrence Kaduri, Aprili 15 mwaka huu.
Mwananchi

No comments: