Lindi. Baraza la Madiwani Halmashauri Lindi, limelaani na kulalamikia kitendo cha watendaji kujiuzia magari na mali za halmashauri hiyo kinyemela bila ya kufuata kanuni na taratibu zilizopo.Malalamiko hayo yamejitokeza baada ya diwani wa Kata ya Kilangala, Halid Chilumba kutoa hoja ya kutaka maelezo juu mpango mkakati wa halmashauri hiyo kuondoa tatizo la upungufu wa usafiri uliopo.
Chilumba alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa usafiri (magari) japo kuwa kuna magari zaidi ya 10 ambayo hayaonekani yakitembea na kufanya kazi za halmashauri.
Alitaja baadhi ya namba za gari hizo kuwa SM 4044 ya Idara ya Kilimo,SM3008 Elimu DFP 4083 DFP 6992,DFP 3014, STK 1380 SM2904.
Mweka hazina wa halmashauri hiyo, Dk Halfani Haule alisema kuwa magari hayo yameharibika na na baadhi ya hayo vipuri vyake haviwezi kupatikana hapa nchini hata nje ya nchi kutokana na muundo wake kutokuwapo na kutokuwa na wataalamu waliobobea katika sekta hiyo. Ahmadi Mbonde Diwani wa Kata ya Mtumbya alisema kuwa kitendo cha magari hayo kuwa mabovu bila ya kupewa taarifa madiwani ni njama ya watendaji hao kutaka kujiuzia wenyewe.
Mbonde alisema kuwa haiwezekani magari yote 10 yakawa mabovu wakati halmashauri imeajiri mafundi kwa ajili ya kufanya marekebisho ya magari hayo.
Sasa ni vizuri madiwani tukaunda tume maalumu ya kwenda kuangalia ubovu wa magari hayo ili kutambua matatizo yake,” alisema diwani Mbonde.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Gress Mbaruku aliwataka madiwani hao kuwa watulivu na kuiachia kazi hiyo Kamati ya Fedha Utawala na Mipango kufuatilia suala hilo.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment