ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 7, 2013

MECHI YA AZAM, BYC II ZAINGIZA MILIONI 44/-

Timu ya Barrack Young Controllers II
Timu ya Azam FC
Mashabiki wa Azam FC wakifuatilia mtanange
Kipre Tchetche wa Azam FC (katikati) akiwatoka mabeki wa Barrack Young Controllers II kwenye mechi ya kimbe la shirikisho iliyochezwa Jumamosi April 6, jiji Dar na timu zote kutoka droo ya 0-0
Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco 'JB' akipiga mpira mbele ya mlinzi wa Barrack Young Controllers II huku wachezaji wengine wakiwa tayari kutoa msaada. (picha kwa (PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

Release No. 058

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 7, 2013


MECHI ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana (Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.
Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.
Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.
Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.
Mechi iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments: