Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar
MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba.
Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fedha kimiujiza dukani na kutokomea, hali iliyosababisha wenye duka kutangaza dau la shilingi 500,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.
Arobaini zake zilipowadia, Rukia alikamatwa akiwa mafichoni, Boko Mtambani na kushushiwa kichapo na wananchi wenye hasirawakimtaka amtaje aliyemtuma.
Baada ya kupokea kichapo, mrembo huyo aliwataja baadhi ya watu akiwemo mganga mmoja anayetokea Sumbawanga (jina tunalo)na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
“Dawa hiyo huwa naiweka kwenye pesa zangu nyumbani ili ziongezeke na nyingine huwa natembea nayo kwa ajili ya kujipatiapesa,” alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo alikiri kufanikiwa kuiba mamilioni ya shilingi kwa kutumia dawa hiyo na kuomba asamehewe. Rukia aliokolewa nandugu zake pamoja na wasamaria wema waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo alikofunguliwa mashtaka ya wizi.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
GPL
GPL
No comments:
Post a Comment