Huyu ndie mtuhumiwa wa mauawaji ya Mwangosi (kulia)
MTUHUMIWA wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)akwama kufikishwa mahakamani baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa.
Mtuhumiwa huyo alipaswa kufikishwa mahakamani hapo jana ila hakufikishwa kabisa.
Mbali ya watu mbali mbali kufika katika Mahakama hiyo ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo bado mahakama hiyo ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo ameshindwa kufika mahakamani leo kutokana na tatizo la ugonjwa linalomsumbua ambapo hata hivyo haijaelezwa mtuhumiwa huyo ana sumbuliwa na nini.
Kutokana na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na ugonjwa hakimu wa mahakama hiyo Mary Senapee alihirisha kesi hiyo hadi Mei 9 itakapofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena.
Kesi hiyo yenye mvuto mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Iringa na watanzania pamoja na dunia kwa ujumla imekuwa ikiendelea kutajwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa na hadi sasa ni zaidi ya mara 12 imekuwa ikitajwa bila kusikilizwea .
No comments:
Post a Comment