Mfanyabiashara na dereva aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam ,leo kesi yake ya tuhuma za kujipatia mali ya Tsh milioni 30 kwa njia ya udanganyifu imeendelea tena.
Mtuhumiwa huyo ambae alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Mwanzo Bomani mjini Iringa wiki mbili zilizopita kesho kupanda tena kizimbani kwa ajili ya kujibu na kuanza kujitetea kwa kesi hiyo iliyopo mbele yake .
Mfanyabiashara huyo Jackson Simbo Stivin(45) alifikishwa awali mahakamni hapo akituhumiwa kujipatia gari aina ya fuso lenye thamani ya Tsh milioni 30 ambalo ni mali ya mfanyabiashara wa mkoani Iringa Venansia Sanga. Kwa mara ya kwanza mtuhumiwa huyo alipofikishwa Hakimu wa mahakamani hiyo ya Mwanzo Bomani Mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 4 mwaka 2012 katika eneo la Miyomboni mjini Iringa . Mheshimiwa Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda kosa hilo alitoweka na kujificha katika mikoa mbali mbali hapa nchini .
Alisema kuwa kutokana na kufunguiliwa kwa kesi hiyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na mlalamikaji waliendelea kumsaka mtuhumiwa huyo bila mafanikio na baada ya kutokea ajali iliyosababisha kifo cha askari huyo wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam katika msafara wa Rais Kikwete ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa baada ya picha yake kuonekana katika vyombo vya habari .
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo dhidi yake na mahakama kudai kuwa dhamana yake ipo wazi na kuwa mdhamini anapaswa kusaini hati ya dhamana ya yenye thamani ya Tsh. milioni 15 masharti ambayo yalitimizwa na wadhamini na mfanyabiashara kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 9 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana .
No comments:
Post a Comment